UCHANGANYAJI WA CHAKULA CHA KUKU

*Kwa wanaochanganya chakula wenyewe hizi ni hatua za kufuata ili kupata chakula chenye mchanganyiko mzuri*

Kwanza inafahamika wengi wanaotumia formula za chakula ,Formula huwa na sehemu kuu mbili


👉 *Macro ingredients* ( malighafi zenye size kubwa kama mahindi, pumba, mtama, dagaa, soya ,alizeti nk

👉 *Micro ingredients* kama (Lysine, Methionine, toxin binder, chokaa, chumvi, premix, mifupa, Dcp nk).


Hivo kwa kuzingatia utaratibu sahihi wa uchanganyaji wa chakula kitaalamu inatakiwa 

👉Micro ingredients (malighafi zenye size ndogo) ndizo zianze kuchanganywa kwanza kisha zifuate zile zenye size kubwa.


 *Hii inazingatiwa kokote uwe unachanganya kwa Chepe/beleshi, Mikono au hata mashineni.* 


Lengo kubwa la kufanya hivi huwa ni kuhakikisha viambata vidogo ambavyo nimuhimu sana kwa kuku vitachanganyikana kwa uwiano sawa kwenye viambata vyenye size kubwa


 *Mfano wa uchanganyaji* 

Mimi *KAHISE* pindi ninapo andaa chakula cha kuku wangu huwa nafuata hatua zifuatazo


 *Moja:* Naandaa malighafi zangu zote na kuziweka eneo nitakapo changanyia


 *Mbili:* Nafanya usafi mahali ambapo nitachanganyia piaa huwa natandika turubai


 *Tatu*  Natayarisha mizani kupimia viambata nitakavyo tumia kutengeneza chakula changu ( *lengo kutengeneza mchanganyiko sahihi kwa vipimo* )


 *Nne:* Naanza uchangaji wa chakula changu hatua kwa hatua kama ifuatavyo



👉Nachukua Dishi/beseni/Kalai na kuviweka viambata vidogo ambavyo nikiweka kwenye turubai vinaweza vikapepea kwa upepo au ikawa ngumu kuvichanganya kama ( *Lysine, Methionine ,toxin binder, chumvi, chokaa, premix, Dcp na mifupa)* hivi navichanganya vikiwa vya kwanza kabisa pamoja ili kupata walau mchanganyiko utakao kua na ujazo unao ridhisha.


👉Baada ya mchanganyiko huo wa kwanza naumwaga kwenye turubai langu na kuanza kuongeza juu yake viambata ambavyo vinaujazo mkubwa 


Mfn: Naweka mashudu nakuchanganya na mchanganyiko wa awali, naweka mahindi paraza na kuchanganya, naweka soya na kuchanganya kisha naweka Pumba na kuchanganya.


Nahakikisha chakula changu nimekigeuza geuza vizuri kwa chepe(beleshi) hadi kujiridhisha kwamba viambata vyote vimechanganyika kwa uwiano sawa 


Kisha nachukua chakula changu na kukiweka kwenye mifuko tayari kwa kutumika na kutunzwa stoo


 *Ila kama upo eneo ambalo mashine za kuchanganyia zinapatikana nivema ukachanganya kwa mashine (Mixer)* 


Hilo ndilo somo langu jipya kwa leo naaamini wengi tutachanganya chakula kwa usahihi sasa🙏🙏

Previous Post Next Post