Swali, Unamaanisha nini unaposema ulinzi wa viumbe hai?
Jibu: Hili nisomo ana ambalo linamfundisha mfugaji namna ambazo atazitumia kuwalinda kuku wake wasipatwe na magonjwa au kwa lugha nyingine ni Viumbe hai salama.
Njia za kuhakikisha ulinzi wa viumbe hai (Kuku).
👉Kuzuia vyanzo vinavyoweza kupelekea vimelea wa magonjwa kufika shambani mfn Panya, Ndege, kuzuia kila mtu kuingia bandani, kuzuia vifaa kutoka shamba moja kwenda kwenye shamba jingine pasipo na kupigwa dawa ya kuua vimelea.
Njia za kuhakikisha ulinzi wa viumbe hai unatekelezwa.
👉Weka sheria za kuzifuata shambani kwako mfn Milango ifungwe unapoingia au kutoka, nyavu zisiwe na matundu ya kuingia ndege au panya kuingia bandani, Iwepo dawa ya kukanyaga mtu anapoingia bandani, viwepo viatu/ mavazi maalumu ya kuingia nayo bandani.
Swali: Unamzungumziaje mfugaji anaefuga katika mazingira ya kawaida na haya uliyoeleza kuhusu ulinzi wa viumbe hai hayafuati je kuna madhara yanaweza kutokea??
Jibu: Madhara yapo makubwa sana kama njia hizi za kuzuia magonjwa hazita fuatwa, kwakua vimelea wataingia kwa urahisi bandani, na kuku wataugua mara kwa mara hii ndio sababu nimeona nianze na somo hili muhimu zaidi.
Shamba litakalo zingatia sheria hizi halita dhuriwa sana ukilinganisha na shamba ambalo halita zingatia njia hizi za ulinzi.
Swali : Kuna aina ngapi za ufugaji wa kuku?
Jibu: Zipo aina kuu na zilizo zoeleka tatu za ufugani wa kuku
Huria -, Kuku wanatoka nje muda wote kutafuta chakula wenyewe na kupewa kiasi kidogo sana cha chakula cha kawaida.
Nusu huria Kuku wanafugwa bandani ila kunakua na uzio ambao kuku watatoka nje na kurudi ndani ( wanapewa chakula sahihi)
Ufugaji wa ndani Kuku wana fungiwa ndani na kupewa mahitaji yote ya msingi muda wote bila kutolewa nje ya banda.
Swali : zipo aina ngapi za kuku?
Jibu : Zipo aina nyingi sana za kuku lakini kwa leo nitazitaja aina kuu nne ambazo kwa wafugaji wengi nchini kwetu wamekua wakifuga katika mashamba yao
Moja.: Kuku wa nyama ( broilers).
Mbili: Kuku wa kienyeji (Asili) mfn Vishingo, kuchi, kuku wa kisukuma nk
Tatu: Kuku chotara mfn Sasso, Kuloirers, Israel, Malawi, Tanbro nk
Nne: Kuku wa mayai mfn Isa brown, Lohmann brown, Hyline, Bavon Brown nk
NB Utofauti wa kuku hao unategemea sana Ukuaji, na uzalishaji na maeneo wanako tokea.
Kitaalamu ushauri wa mfugaji afuge kuku aina gani unategemea sana na maeneo alipo na uhitaji wake wa soko upoje mfn Kama uhitaji ni wa kuku wa kienyeji ukifuga broilers Soko itakua shida kwako HIVO LITAMBUE SOKO
TUHAMIE KWENYE CHANJO
Swali: Je zipi ni chanjo za muhimu za kufuata kwa kila aina ya kuku uliyo ifundisha hapo awali
Kwanza kabisa mfugaji aelewe chanjo sio tiba ila ni kinga ya kuzuia uwezekano wa ugonjwa fulani kuto tokea hasa magonjwa ya virusi.
Ratiba za chanjo
1. BROILERS
siku ya 7 na 21 newcstle
Siku ya 14 gumboro
Au
Siku ya 7 newcastle
Siku ya 14 na 21 Gumboro
wa
👉Kuku chotara,na kuku wa mayai
Siku ya 1 Mareks
Siku ya 7 na 21 newcastle
Siku ya 14 na 28 Gumboro
Siku ya 30 ( wk 4-5) ndui.
Kila baada ya miezi mitatu newcastle
Kuku wa kienyeji
Siku ya 7 na 21 newcastle
Siku ya 14 na 28 Gumboro
Siku ya 35 Ndui
Kila baada ya miezi mi 3 newcastle
NB RATIBA ZA CHANJO ZIZINGATIWE.
Swali: Je kama mfugaji hatawapa kuku chanjo dawa hizi za asili zitasaidia kuzuia hayo magonjwa?
Jibu :Hapana inapaswa chanjo zifanyike ndipo tiba nyingine zilizo thibitishwa ziendelee usitumie dawa ya asili kama kinga dhidi ya magonjwa. NB chanjo hazina uhusiano kabisa na Tiba.
Namna za kuzuia magonjwa.
Namna kubwa kabisa ni kuzingatia ulinzi wa viumbe hai, na kikubwa hapa USAFI UZINGATIWE
👉Vyombo vya chakula na maji
👉Chakula
👉Bandani kiujumla
👉Banda lisafishwe na kupuliziwa dawa kabla ya kuingiza kuku na likae wiki 1 -4 kupoteza vimelea
👉Ubora wa chakula na ujiandae kugharamia chakula kwa kipata malighafi salama zisizo na uvundo, kavu kuzuia fangasi na bakteria kwa kiwango kikubwa