MADINI YA PHOSPHORUS NA CALCIUM


 TUJIFUNZE KUHUSU MADINI YA CALCIUM NA PHOSPHORUS.

Kwa kipindi kirefu tumekua tukiambizana juu ya madini hasa ya calcium na Phosphorus  kwenye chakula cha  kwamba yanaweza sababisha 

👉kuku kushindwa kusimamama (kulegea miguu)

👉Mayai kuwa malaini (gamba laini)

👉Mayai kuwa na vidot dot vyeupe kwenye ganda

👉Kuku kula mayai

👉Kuku kudonoana n.k

 Ni kwanini haya yote hutokea?

Kwanza kabisa kwenye chakula cha kuku ukiachana na vyanzo vingine vya chakula kama Wanga, Vitamin , Protin, na mafuta,,, *MADINI* yanachukua sehemu yake kubwa sana katika kuhakikisha ukuaji na uzalishaji wa kuku unakua sahihi.

Leo nitoe somo kuhusu Calcium na Phosphorus

Haya ni madini muhimu na yanayo hitajika kwa kiwango kikubwa katika kuhakikisha kuku wanakua imara.

Yanasaidia kuimarisha 

👉Mifupa

👉Ganda la yai

👉Kuimarisha misuli nk

Hivyo ni muhimu mfugaji pindi achanganyapo chakula cha kuku wake, aweke viambata ambavyo vitafanya kuku apate madini hayo muhimu

Miongoni mwa vyanzo vya madini hayo muhimu ni kama

👉Di calcium phosphate DCP

👉Mono calcium Phosphate MCP

👉Mifupa

👉Chokaa

👉Konokono n.k

 Angalizo

 Matumizi ya Konokono na mifupa iliyo andaliwa katika mazingira ambayo sisalama imeripotiwa kusababisha magonjwa hasa typhoid kwa kuku ( pindi unapo amua kutumia zingatia sana usafi na ubora wake.)

Kwanini Calcium na Phosphorus sana na si madini mengine kwa leo

Haya ni madini ambayo yanahitajika kwa kiwango kikubwa katika stage zote za ukuaji wa kuku na yanahitajika kwa kiwango tofauti tofauti 

 Mfn:

Kuimarisha mifupa (Stage zote) za ukuaji

Kuimarisha ganda la mayai pindi wanapo anza kutaga na wanapoendelea

Balance ya madini hupunguza case za kudonoana na kula mayai

 Kuna swali huwa naulizwa sana  Kwanini tusiweke aina moja wapo ya malighafi kupata kiwango kinacho hitajika kwa kuku.

Jibu:Kiwango cha malighafi kuwekwa kwenye vyakula kila ukomo wake hasa DCP na MCP, ukizidisha hasa kwa vifaranga na kuku wanao taga huonesha madhara haya ya kinyesi kuganda nyuma au vidot vidot vingi kwenye mayai kila siku mfululizo.

Kwahiyo basi kutokana na hofu ya ubora na kukosekana kwa vipimo vya ubora maeneo mengi huwa tunaweka mchanganyiko wa malighafi kadhaa ili kukidhi uhitaji kitaalamu na kwakuangalia urahisi wa upatikanaji wa malighafi.

 Kitaalamu unaweza kulisha kuku kwa namna tofauti 

👉Kununua chakula cha kampuni flani

👉Kutumia chakula cha kampuni na kisha baadae kuchanganya Mwenyewe.

👉Kuchanganya chakula mwenyewe mwanzo hadi mwisho.

Previous Post Next Post