MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE.

👈NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO

_Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. 

Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani

_Tiba_ : Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus

👉kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia antibiotic kuzuia maambukizi ya pili (secondary infection).

Kinga: Chanjo ya newcastle siku ya 7 na 21 na kila baada miezi mitatu.

👈 GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE

_Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa

PM : Uvimbe kwenye bursal of fabricus 

_Tiba_ :Hakuna tiba ni ugonjwa wa virus. 

Kinga: Chanjo ya Gumboro siku ya 14 na 28

👈 MAREK'S DESEASE/ MAHEPE

_Dalili kuu_:kuparalyse /kukakamaa  kwa miguu na mbawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kiifadhia chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5/wakianza kutaga.

_Tiba_ :Hakuna tiba ni ugonjwa wa virus. 

 Kinga:  Kuku wapewe chanjo ya mareks siku ya kwanza 

👈NDUI YA KUKU / FOWL POX.

_Dalili kuu_:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya kama vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni. 

_Tiba_:Hakuna tiba ni ugonjwa wa virus,

👉 kupunguza madhara muoshe kwa maji ya uvugu vugu hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic kama Otc 20%.

Kinga:  Kwa kutegemea eneo unapo patikana kuku wachanjwe chanjo ya Fowl pox ( wiki ya 4-5) hasa siku 30, japo kunatafuti zinaendelea kufanywa kuweza kuchanjwa mapema zaidi. 

👈 MAFUA MAKALI/ CORYZA

_Dalili kuu_:Chafya, kukohoa, kusinzia, kuvimba uso/kichwa /macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, urenda puani na mdomoni.  Ugonjwa huu hufanana sana dalili na upungufu wa vitamin A ,hivo unahitaji Daktari kuubaini na kuutibu mapema ( kwa takwimu za sasa ni ugonjwa 

Ambao unaua sana kuku).

_Tiba_ : Fluban, au  tylodox , Enrovet , au dawa zenye Enflolaxacin  uchaguzi wa dawa uangalie kiwango cha ugonjwa kuepusha vifo ( mshirikishe Daktari).

Kinga: Chanjo ya infectious corryza wiki ya 8-9 (upatikanaji wake mgumu kidogo kama utahitaji usaidizi nitafute).


👈 FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO

_Dalili Kuu_:Mharo rangi ya mchanganyiko hasa nyeupe yenye mchanganyiko na njano na wakati mwingine kijani kiasi.

Kuku anapunguza sana uzito na kukonda , mfupa wa kifuani huchongoka na kuwa mwembamba sana.

_Tiba_: Esb3, Trimazine 30%, Tylodox, Trisumysin, Biosol  Trisul ,Enrovet, Ganadexil, Limoxin nk 

Kuzuia: Jitahidi kuku wako waishi kwenye banda safi, wale chakula kisafi na maji safi,  Nunua vifaranga kutoka shamba lenye wazazi salama wasio na typhoid kwani huambukizwa kwenda kwa vifaranga.

👈 COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU

_Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu. 

PM : Damu kwenye utumbo wa kuku

Kuzuia : Banda liwe kavu na usiruhusu unyevu mwingi bansani

_Tiba_: Dawa nzuri ni Amprolium 20%,nyingine ni Esb3, Trimazine 30%, vitacox, na agracox, Vetacoxy, Anticox N.k. Uchaguzi wa dawa uzingatie leval ugonjwa ulipo fikia ( Mwone Daktari ).

👈 _BUMBLE FOOT, UGONJWA WA MIGUU_

Huu ugonjwa unawapata kuku na miguu sehemu ya kukanyagia huvimba na kujaa usaha wakati mwingine

Husababishwa na bakteria Staphylococcus  kuku hushidwa kutembea

Tiba na kuzuia: Wape antibiotic kama Otc, pia vitamins na hakikisha kuku wako wanaishi kwenye banda lenye Randa.

MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKANA NA LISHE DUNI

👈Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.

_Tiba_ : Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa vitamin, madini, na protein, kwa wanaodonoana kama utahudumia kwa vitu vingine na wataebdelea kudonoaba ( kata au choma midomo yao. )

NOTE;;: Uchaguzi wa dawa au utambuzi wa kujua magonjwa unahitaji utaalamu na uzoefu mkubwa ili kuzuia kasumba ya kutibu magonjwa kwa kubuni, ni vema sana Uwapeleke kuku Clinic au uwasiliane na madaktari waliopo karibu yako kupata msaada wa zaidi na wa haraka.

Magonjwa yapo mengi sana siwezi kuyamaliza niwe nimetoa somo kwa sehemu naamini umenifunza kitu kikubwa.

Previous Post Next Post