Kutokana na ukweli kwamba vifaranga hasa wa chini ya mwezi mmoja na nusu wamekua wakipata changamoto hasa za mafua , mafua makali, na upungufu wa vitamin A
Dalili zao zikiwa zina fanana kwa kiasi kikubwa sana ikiwa
👉Kupiga chafya
👉Jicho moja au yote kuvimba
👉Ute kujaa mdomoni
👉Macho kutoa machozi
👉Kuku kushindwa kuhema n.k.
Kwa wafugaji wengi changamoto hii imekua msiba mzito unaofanya kupoteza idadi kubwa sana ya vifo.
👆Kwa kuwa nimekuwa nikiletewa case hizi mara kwa mara, niliamua kufanya juhudi za makusudi kutafuta nini haswa kitakua kisababishi kikuu
Na nilipo pewa malalamiko hayo niliomba mfugaji apige picha, au video fupi ya kuku wake na mwonekano wa banda lilivo jengwa.
Majibu ya utafiti
👉Waliojenga mabanda bora yenye kuruhusu hewa kuingia na kutoka hawakuwa na changamoto hii kwa kiasi kikubwa sana kuliko walio acha madirisha madogo kuzuia hewa kuingia na kutoka
👉Hivo ninashauri mfugaji, ujitahidi kujenga banda litakalo kuwa rafiki kwa kuku wako, najua wengi huhofia kuibiwa ila tuangalie pande zote mbili kuku wanakufa sana na hii ni hasara.
👉 Walio wapa kuku vitamins kwa wingi tangu wakiwa wadogo wamekua wakipata changamoto hii kwa kiasi kidogo kuliko ambao hawakuwapa vitamins vizuri kuku wao.
Nashauri ratiba ya vitamins kama utaweza fuata hii ambayo nimekua nikiitumia na imwonesha manufaa kwa kuku wangu.
👉Siku 1-5 Neoxychick, au Tetracolivit au Multivitamin yoyote yenye kiwango kidogo cha dawa kukausha vitovu na iwe na madini.
👉Siku ya 8-13 tumia vitamins kama Amintoto, Dad Octavit, Tetravit n.k ( Tumia vitamin yenye kiwango kikubwa cha Vitamin A na Vitamin K3)
👉Siku ya 15-20 tumia vitamin kama Amintoto, Amylyte, Vitalyte, n.k ( Vitamin zenye kiwango kikubwa cha Vitamin A na K3)
👉Siku 22-28 Tumia Introvit A , Farm vita au vitamin yoyote yenye kiwango kikubwa cha Vitamin A na K3, Baada ya hapo unaweza kuwa unawapa vitamin walau mara kila baada ya wiki mbili case hizi zitapungua kwa kiwango kikubwa.
👆Kwanini nimeongelea sana Vitamin A na K3, nikwasababu vifaranga husumbuliwa sana na matatizo ya uono hafifu pia kiwango kikubwa cha magonjwa hasa ya kuhara damu ( hivo K3 husaidia sana mfumo wa kinga )
Kwa wewe unaeanza kufuga vifaranga jitahidi kuzingatia utaratibu huo wa vitamins itakufaa sana.
👉Kingine cha muhimu nilicho ona ni sababu kubwa ya mafua, ni kuchukua randa moja kwa mojakupeleka bandani walipo kuku,👈Jitahidi randa zikae walau wiki moja zipunguze harufu na vumbi ndipo uwawekee kuku ( zitayarishe ukiweza zitandaze kwenye trubai zitoe vumbi na harufu ya kupalia au kuzichekecha ).
