*BIO SECURITY*
👆Bio👉Viumbe hai
👆Security👉Usalama
Kwa mjumuisho, Biosecurity..ni *viumbe hai salama*
Yaani jumla ya mambo yote yatakayo fanyika kukinga magonjwa yasiingie kwenye shamba la kuku.
*UGONJWA KUINGIA SHAMBANI UNATEGEMEA YAFUATAYO*
👉Port of entry/njia ya kuingia
👉Resevoir host/Anaetunza vimelea bila kuumwa
👉Succeptible host/ mnyama atakae ugua
👉Port of exit/Njia ya kutokea
👆Port of entry/uingiaji
Hii ni mianya yote ambayo ugonjwa unaweza kuingia shambani, mfano
👉Wanunuzi wa kuku
👉Vifaa vya kusafirishia bidhaa kuja au kutoka shambani
👉Wataalamu au madaktari
👉Watu wasio na ulazima kuingia bandani
👉Mavazi yasiyo rasmi
👉Ndege, Panya, vyakula visivyo safi
👆Hivyo ni baadhi ya vyanzo ambavyo huweza kuleta ugonjwa kuingia shambani
*SULUHU*
👉Uwe na mavazi maalaumu ya kuingilia bandani
👉Wageni wasio na ulazima wasiingie bandani (waishie nje ya banda)
👉Madaktari wanaotembelea mradi, wawe na mavazi maalumu ya kujikinga, wasiwe wametoka kwenye shamba lenye ugonjwa, na akifika aanze kupitia kuku ambao hawaumwi na wale wanao umwa wawe wamwisho kabisa( zingatia).
👉Wanunuzi wakija, sio wote waingie shambani, kumbuka hawa hutembelea mashamba mengi hivo huwa wasababishi wazuri wa kubeba ugonjwa kutoka point A-B-C ( *Zuia wasifike na Kuku kutoka shamba jingine kuja nao kwenye shamba lako* )
👉Ziwepo dawa za kunawa mikono (sanitizer), na Dawa za kukanyaga kabla ya kuingia bandani
👉Kuwe na utaratibu maalumu wa kuteketeza mizoga ya kuku waliokufa....hayo ni baadhi.
👆Resevoir Host(mbebe vimelea asie ugua).
👉Huyu ni kiumbe yoyote anae weza kubeba vimelea vya ugonjwa ila yeye asiugue
Mfn.
Ndege pori-Mafua
Kuchanganya makundi ya ndege tofauti mfn-Bata na kuku( kitaalamu hairuhusiwi)
Panya-Salmonella
Viroboto, utitiri, mbu nk
*Hawa kwa namna yoyote wanatakiwa kudhibitiwa kuto ingia bandani...kupunguza kasi ya maambukizi.*
👆Succeptible host( Kuku mwenyewe)
👉Huyu ni kiumbe ambae ataugua ugonjwa, au ataonesha dalili za maambukizi, mara baada ya vimelea kuingia shambani utapita muda ( incubation period) kisha vimelea watakua wamezaliana kiasi cha kupelekea infection na hatimae ugonjwa
🤛 *Hivo hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa ili kudhibiti vyanzo vya ugonjwa visiingie.*
👆Port of exit/Utokaji wa ugonjwa
👉Kwa namna gani ugonjwa unaweza kutoka shambani,
👆Mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa,
👉Mayai yaliyotoka kwa kuku anaeumwa
👉Vifaranga waliotoka kwa kuku anaeumwa
👉Kuku wanao uzwa kwenda mahala pengine.
Hivo nimihimu sana mfugaji ukawa unafahamu Chanzo cha kuku wako ili kuepuka matatizo yanayo weza kuzuilika
Tags:
MBINU ZA UFUGAJI
