Kuku wanaopata lishe bora, kutunzwa
vizuri na kupatiwa chanjo
dhidi ya magonjwa yanayotokea mara kwa
mara huwa na afya nzuri.
Ni bora kuzuia magonjwa kuliko kutibu
ili kupunguza vifo na gharama.
Iwapo ugonjwa utatokea kuku wagonjwa
watenganishwe na kuku
wasio wagonjwa na wapatiwe tiba.
Kanuni muhimu za kufuata ili
kuzuia magonjwa ni:-
Banda liwe safi muda
wote,
Kabla ya kuweka kuku,
banda linyunyuziwe dawa ya kuua
wadau wa magonjwa mbalimbali,
Kuku wakaguliwe kila
siku ili kubaini wagonjwa au wenye
matatizo, kuwatenga na kutoa taarifa kwa
mtaalam wa mifugo,
Kuku wapatiwe chanjo
dhidi ya magonjwa mbalimbali,
Watu wasiohusika
wasiingie eneo la kufugia kuku bila utaratibu,
Ndege na wanyama
wengine wasifike eneo la kufugia kuku,
Banda la kufugia kuku
litenganishwe na mabanda ya mifugo
mingine,
Lango la kuingia katika
banda la kuku liwekewe dawa ya
kukanyaga kwa wanaoingia ndani ili
kuzuia kuingiza vimelea
vya wadudu wa magonjwa;na
Vifaa vya chakula na
maji viwe safi wakati wote.
Dalili za
Kuku Mgonjwa
Dalili za
ujumla zinazoonekana kwa kuku mgonjwa ni kama
zifuatazo:-
Kuzubaa,
Kupoteza hamu ya kula,
Kujitenga na wenzake
katika kundi; na
Kupunguza au kusimama
kutaga.
Mfugaji anapoona mojawapo ya dalili hizo
atoe taarifa kwa mtaalum wa
mifugo
Ufugaji wa Aina Nyingine za Ndege
Aina ya ndege wengine wanaofugwa nchini
Tanzania ni pamoja na Bata
maji,Bata bukini, Kanga na Njiwa. Ndege
hao hufugwa kwa
kiasi kidogo ukilinganishwa na kuku kwa kuwa
soko lao ni dogo.
Utunzaji
wao hautofautiani sana na kuku;
Wajengewe banda la
kuishi ambalo ukubwa wake utagemea idadi ya
ndege wanaofugwa,
Wapatiwe chakula chenye
virutubisho na maji ya kunywa yakutosha,
Wapatiwe kinga na tiba
dhidi ya magonjwa,
Bata maji na Bata
bukini wajengewe bwawa lenye nafasi ya
kukutosha kwa ajili ya kuogelea; na
Njiwa wajengewe viota
sehemu ya juu kama kwenye mapaa ya
nyumba.
Utunzaji
wa Kumbukumbu
Utunzaji wa kumbukumbu ni muhimu sana
katika ufugaji wa kuku na
ndege wengine wafugwao ili kusaidia
mfugaji kujua maendeleo ya
ufugaji wake. Utaratibu wa kuweka
kumbukumbu mara tukio linapotokea
ni lazima ili kuepuka kusahau.Mfugaji
ahakikishe anaweka kumbukumbu
ambazo ni sahihi na zinazoeleweka.
Aina za
Kumbukumbu
Kumbukumbu zinazopaswa kuwekwa ni pamoja
na:-
Aina na idadi ya kuku
waliopo kwenye kila kundi (mfano
vifaranga,wanaokua,wanaotaga,majogoo),
Uzalishaji wa mayai kwa
kundi la kuku waliopo,
Utotoaji wa vifaranga,
Kinga na matibabu,
Mapato na matumizi,
Utagaji wa kila kuku na
utunzaji (kwa kuku wa asili); na
Kumbukumbu za vifo.
Chakula na uchanganyaji wake
Chakula ndicho huchangia sana katika
gharama za uzalishaji kwa
zaidi ya asilimia 60. Na gharama ya
chakula huongezeka kila mwaka
kuliko hata gharama za mayai au kuku
wenyewe.
Mfugaji anaweza kununua chakula
kilichochanganywa au
kuchanganya mwenyewe. Ila anapaswa
kuzingatia virutubisho na
viini lishe vilivyopo katika chakula
hicho pia kuzingatia mahitaji ya
kuku wake.
Virutubisho vinavyotakiwa ni vingi
lakini vimegawanywa katika
makundi sita ya vyakula ambavyo ni;
protin, wanga, mafuta,
madini,vitamini na maji.
Protini inahitajika kujenga mwili wa
kuku.
Ni muhimu kwa ukuaji wa kuku, uzalishaji wa
mayai na kuimarisha afya. Wanga na mafuta
vinahitajika ili kuupa mwili nguvu na
joto na kuwezesha mwili kufanya
kazi zake ipasavyo. Vitamini
vinahitajika ili kumwezesha mwili wa
kuku kufanya kazi zake vizuri. Madini
yanahitajika ili kuimarisha
mifupa na uzalishaji.
Tags:
MAGONJWA YA KUKU