Sifa za kuku bora wa mayai na nyama

Kuku wa Kisasa
Kuku bora wa kisasa kwa ajili ya mayai au nyama ni mwenye sifa
zifuatazo:-
1.    Uwezo wa kuanza kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 5-6)
kutegemea na koo,
2.    Umbo kubwa na anayekula haraka (kilo 1.5-2.0 kwa kipindi cha
wiki 8-12 kutegemea na koo kwa kuku wa nyama,
3.    Anayetaga mayai mengi (250 au zaidi) kwa kuku wa mayai kwa
mwaka; na
4.    Awe na uwezo wa kutaga katika umri wa miezi 6-8.
2.3 Uchaguzi wa Jogoo Bora wa Mbegu
Jogoo wa mbegu anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
Ø  Achaguliwe kutoka kwenye koo zenye sifa ya kutaga mayai
mengi,
Ø  Mrefu, umbo kubwa, miguu imara na yenye nguvu,
Ø  Awe machachari, ushawishi kwa mitetea na ari ya kupanda
Ø  Uwezo wa kupanda akiwa na umri wa miezi 7-10.
 Mayai kwa Ajili ya Kutotoa Vifaranga
 Uchaguzi wa Mayai
Mayai kwa ajili ya kutotoa vifaranga yawe na sifa zifuatazo:-
*     Yaliyorutubishwa na jogoo,
*     Yasiwe na nyufa,
*     Yasiwe na maganda tepetepe,
*     Yasiwe na kiini kilichovunjika,
*     Yawe na ukubwa wa wastani; na
*    Yasiwe yamekaa zaidi ya wiki 2 baada ya kutagwa.
 Utunzaji wa Mayai
Mayai ya kienyeji kwa ajili ya kutotoa vifaranga yatunzwe kwa
kusimamishwa wima sehemu iliyochongoka ikiwa imeangalia chini kwa siku
3za mwanzo na kisha yageuzwe ili sehemu iliyobutu iangalie chini. Mayai
yahifadhiwe kwenye sehemu iliyo na ubaridi kidogo na giza.

Previous Post Next Post