Zifahamu kanuni muhimu katika kuchimba bwawa la samaki

Image result for bwawa la samaki
Hatua za muhimu katika uchimbaji wa bwawa

  1.        Fyeka mahali pa kujenga bwawa.
  2. Pima bwawa na weka mambo.
  3.   Ondoa udongo wa juu (mbolea, mchanga, mizizi n.k.) na weka pembeni.
  4. Chimba msingi wa kuta; upana futi 1 na kina futi 1½.
  5. Jaza huo msingi kwa udongo wa mfinyanzi na kuushindilia. Hii itasaidia kupunguza kunywea kwa maji.
  6. Anza kuchimba bwawa na kujenga kuta kwa kutumia udongo tu (bila mchanga, mawe, miti, mizizi n.k.) ili kupunguza kunywea kwa maji kutoka bwawani baada ya kulijaza.
  7. Shindilia kikamilifu udongo unaowekwa kwenye kuta.
  8. Jaribu kusawazisha juu ya kuta na chonga kuta ziwe na mtelemko wa kiasi, zisiwe wima kwani zitamomonyoka kirahisi.
  9.   Chonga sakafu ya bwawa kwa kuiwekea mteremko wa kiasi kutoka upande wenye kina kifupi kwenda upande wenye kina kirefu..
  10. Weka bomba la kuingizia maji na bomba la kuondolea maji bwawani.
  11. Rudishia udongo wa juu uliouondoa hapo awali kwenye kuta za bwawa.
  12. Panda majani yanayotambaa  kama mbudu ukutani kuzuia mmomonyoko.
  13. Jenga wigo wa kuweka mbolea ya samadi au Mbuji ndani yake
  14. Jenga uzio, seng’enge au panda miti yenye miba kuzunguka bwawa kuzuia maadui wa samaki kuingia bwawani.
  15. Tawanya mbolea na majivu chini ya bwawa ili kuua wadudu wanaoweza kuwamo ndani ya bwawa kabla ya samaki kupandwa bwawani.
  16. Baada ya hatua hizo kukamilika, sasa jaza maji bwawani.
Previous Post Next Post