MAMBO MUHIMU KATIKA KUCHAGUA ENEO LA KUJENGA BWAWA
1.
Maji ya kutosha ni yale yanayoweza kujaza bwawa lako
ndani ya siku chache. Pia maji hayo yawe ni ya kuaminika ili wakati
unapoyahitaji, yapatikane. Chanzo chaweza kuwa mto au chemichemi. (Maji ya mvua
hayaaminiki, wakati yale ya bomba ni ya ghali sana kutokana na kuyalipia kwa
mamlaka husika)
2.
Udongo unaofaa ni ule unaotuamisha maji, kama vile wa
mfinyanzi au mchanganyiko wa mfinyanzi na tifutifu. Mchanga mtupu haufai kwani
huruhusu maji kunywea kirahisi.
3.
Mteremko ni vema usiwe mkali sana, ila uwezeshe maji
kutiririka kuingia na kutoka bwawani. Eneo la tambarare kabisa si zuri sana,
kwani utafanya uchimbaji wa bwawa kuwa kama kisima na haitakuwa rahisi kuondoa
maji toka bwawani itakapo hitajika ambalo si zuri kwa ufugaji bora
wa samaki.
4.
Ni vizuri eneo liwe karibu na nyumbani ili kudhibiti wezi
na maadui wa samaki, pia huwezesha kutoa huduma kwa urahisi.
CHAGUO LA UMBO NA
UKUBWA WA BWAWA
1.
Umbo na ukubwa wa bwawa hutegemea sura na mwinuko wa eneo
husika na eneo alilonalo mfugaji.
2.
Kwa kawaida umbo lolote hufaa kwa uchimbaji wa bwawa,
lakini, ili kurahisisha uvunaji, umbo mraba au mstatili upendekezwa zaidi.
3.
Vile vile, ukubwa wa bwawa hutegemea ukubwa wa eneo
husika, uwingi wa maji na uwezo wa mkulima.
4.
Bali, ili kupata pato la kuridhisha na kurahisisha
utoaji huduma kama vile kulisha, inapendekezwa kuwa ukubwa wa bwawa ni vema
liwe na upana wa kati ya mita 10 na mita 20 na urefu wa kati ya mita 20 na mita
30. Umbo la mraba au mstatili huvutuia zaidi.
Tags:
UFUGAJI SAMAKI