Zijue kanuni za ufugaji kondoo na tabia zake

Ufugaji wa kondoo

UFUGAJI KONDOO
Kama walivyo mbuzi, kondoo pia wanaweza kufugwa na wafugaji wadogo wadogo na kwenye eneo dogo ambalo hutumika kwa kilimo pia. Kwa kuzingatia yafuatayo, mfugaji wa kondoo ataweza kuwa na ufanisi mzuri.
Kondoo hupenda kujilisha kwenye makundi
Kondoo hupenda kujilisha kwenye makundi
Banda la kondoo
Banda na malazi ni lazima yawe mazuri na
v  Lenye nafasi ya kupitisha hewa vizuri,
v  Linaloweza kuwakinga mifugo dhidi ya mvua, jua na upepo.
v  Sakafu iliyo nyanyuka ni nzuri zaidi.
Sehemu ya mbele ya banda iwe na uwazi.
v  Inashauriwa sakafu iwe na mwinuko kidogo.
Usafi
Ni lazima Uchafu utolewe kila siku ili kuweka banda katika hali ya usafi na ukavu kila wakati. Hii, itasaidia kuzuia magonjwa ambayo hushambulia kondoo mara kwa mara kama vile:
v   Pneumonia
v  kuoza kwato
v  kupunguza uwezekano wa kuwepo wadudu nyemelezi.
Kwa kondoo wanaofugwa nusu ndani nusu nje, banda la kawaida lililoezekwa linatosha kuwasitiri kondoo nyakati za usiku. Tenga walau  mita za mraba 1.5 kwa kila mnyama ili kuzuia uwezekano wa magonjwa yanayotokana na msongamano.
Kwa kondoo wanaolishwa ndani(zero grazing), inatakiwa:
1)      Sehemu kavu, banda lenye hewa na kuezekwa vizuri (skwea mita 2)
2)      Kihondi kizuri cha kulishia ili kufanya malisho kuwa safi na kupunguza uharibifu.
3)      Sehemu nzuri ya nje inayowafaa kondoo kutembea.
4)      Tenga walau skwea mita 3 kwa kila kondoo. Kila mwanakondoo anahitaji eneo la kutosha kwa ajili ya kukimbia na kucheza.
 
5)      Maji safi na jiwe la chumvi vinahitajika kuwepo wakati wote.
 
6)      Utahitajika kuwa na banda la ziada ama kwa muda kwa ajili ya kondoo wenye mimba, kuzalia na kwa ajili ya wanakondoo. Pia, kwa kondoo wanaoumwa.
Banda la uzio kwa ajili ya kondoo unaweza kuwa rahisi zaidi kwa kuwa kondoo hawaruki wala kupanda juu.
Virutubisho kwa ajili ya kondoo
Kondoo hutumia muda mwingi wakati wa mchana kula majani na baadaye hucheua na kutafuna. Wanapendelea zaidi kula majani na vichaka ambavyo vina mchanganyiko wa madawa ya asili. Wanakondoo hujifunza kutoka kwa mama zao ni nini chakula. Kama unawaanzishia aina mpya ya chakula, lisha kwa kiasi kidogo na uweke kwenye sehemu walikozoea kulishiwa.
Kuwa makini na ukumbuke kuwa wanyama wanaopata lishe duni ni rahisi kushambuliwa na magonjwa na hawana uwezo wa kukabiliana na vimelea vya magonjwa. Uzalishaji wa maziwa pia huwa kidogo kiasi cha kufanya watoto wake kuwa dhaifu na kukua kwa shida.
Previous Post Next Post