Ufugaji kuku wa asili


Kwa kawaida  ili kupata kuku wengi kwa muda mfupi tetea lazima atengwe na vifaranga arudishwe kwenye kundi lenye jogoo, atapandwe

na kurudia kutaga mapema.

Kwa kawaida vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na baridi,kuliwa na wanyama wengine na magonjwa.

Ili kudhibiti magonjwa, vifaranga wapewe chanjo dhidi ya magonjwa yafuatayo:

a. Kideri ( New castle) siku ya 3-7 baada ya kuanguliwa, rudia baada ya wiki tatu kisha

uchanje kila baada ya miezi mitatu.

b. Kuhara damu au rangi ya ugoro (Coccidiosis) : Wapewe kinga kwa dawa ya

Amprolium kwa siku 3 mfululizo wanapofikisha umri wasiku 7 baada ya kuanguliwa.

c. Gumboro wanashusha mbawa na kujikusanya pamoja kwa baridi, pia wanaharisha

nyeupe.Hutokea kuanzia wiki ya 2 hadi ya 18.Wapewe chanjo siku ya 10-14

baada ya kuanguliwa na rudia baada ya siku 28 na 42. Kwa magonjwa mengine

angalia maelekezo sehemu ya magonjwa ndani ya mwongozo huu.

Vifaranga wapewe chakula kilichoelezwa katika sehemu ya tatu ya kijitabu hiki na

maji safi ya kutosha wakati wote kwa muda wa miezi miwili. Baada ya hapo wanapewa

chakula cha kuku wanaokua.

Kuku wakikaribia kupevuka wakiwa na miezi mitatu hadi minne tenganisha temba

na majogoo ili kudhibiti kuku wenye uhusiano wa damu wasipandane wao kwa wao.

Wakipandana na mayai yao yakianguliwa hawatatoka vifaranga wenye sifa nzuri mfano:

ukuaji wao utakuwa hafifu kuliko wazazi wao, uwezo mdogo kuhimili magonjwa na

wengine wanaweza kuwa na ulemavu.

 Kumbuka;Pia zingatia matemba hao wasipandwe na baba

yao. Vilevile majogoo hao wasimpande mama yao.

.................................................................................................................................................
Previous Post Next Post