Mbinu za kupata soko

Mbinu za kupata soko
Mbinu zaidi ya kupata masoko mazuri

Umoja wa kuzalisha na kuuza

Kwa kawaida kama bidhaa ina soko, wateja hupatikana kwa urahisi pale wanapohakikishiwa

upatikanaji wa bidhaa kwa wingi katika sehemu moja.

Katika hali hii, wanunuzi huwa tayari hata kununua kwa bei ya juu zaidi kwa sababu ya

kupunguza muda na gharama ya kutafuta bidhaa ya kutosha kupeleka sokoni.

Kwa upande wa kuku jambo hili linawezekana kama mfugaji atafuga kuku wengi wa umri

usiopishana sana kwa wakati mmoja. Watakapofikia kimo kinachofaa kuuza utawauza

wengi kwa wakati mmoja na kwa faida zaidi.

Mahali ambapo mfugaji mmoja mmoja hawezi kukidhi wingi wa hitaji la wanunuzi,

wafugaji kadhaa wanaweza kuunda umoja wao wa kuzalisha (kila mmoja kwake ) na

kuuza kwa kipindi kimoja na kupata faida zilizotajwa hapa juu.

Faida nyingine ya kuuza katika umoja ni kuongezeka kwa uwezo wenu wa kupanga na

kusimamia bei mnayotaka kuuzia. Sauti na uamuzi wenu wa pamoja utawapa nguvu ya

kusimamia bei yenu mnayoipanga dhidi ya bei za chini wanazotaka wanunuzi. Uwezo

wako wa kusimamia bei unyoitaka ni mdogo ukiuza peke yako.
Previous Post Next Post