Masoko

Masoko ya kuku
Ufugaji kuku

Masoko

 Mambo kadhaa ya msingi

yatakayomsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara

unayoifanya:

Kwanza kabisa jiulize kama bidhaa unayozalisha ina soko? Na kama soko lipo:

• Lipo wapi na hali ya miundombinu za kulifikia iko vipi ( ili afahamu gharama ya kufika

sokoni kama utaamua kuuzia sokoni).

Bidhaa inahitajika kwa wingi kiasi gani na wakati gani sokoni

• Soko linahitaji bidhaa yenye sifa zipi ( ubora n.k. ili uzalishe sawa na matakwa ya soko

n.k)

• Kama wanunuzi watakuwa na utayari kununulia unakozalishia, je unao uwezo wa

kutosheleza mahitaji yao (ili uweze kujipanga kukidhi mahitaji kwa kuongeza uzalishaji

au kwa kuungana na wazalishaji wengine).

• Linganisha bei ya bidhaa sokoni na bei ya kuuzia unakozalishia (ili ujue palipo na faida

zaidi kwako baada ya kuondoa gharama za kufuata soko) Ila ukiamua kuuzia sokoni

hakikisha unao uwezo wa kushindana na wauzaji wengine huko sokoni.

Majibu ya maswali haya ndiyo yatakayokupa msingi wa kujipanga kiuzalishaji ili hatimaye

upate faida. Hivyo hata kabla hujaanza kuzalisha fahamu haya yaliyotajwa hapa juu.

Kutafuta na kutumia taarifa za masoko ya sehemu tofauti

Kwa kadri utakavyokuwa unaendelea kuzalisha, mabadiliko mbali mbali yatatokea

kuhusiana na uzalishaji wako na hata kuhusiana na soko la bidhaa unayozalisha kwa

maana ya kuku.

Ili uendane na mabadiliko yanayotokea ni muhimu mzalishaji upate taarifa za hali ya

soko mara kwa mara. Taarifa hizi zitakusaidia kufanya maamuzi yatakayokuwezesha

kuendelea kupata faida.

Taarifa za masoko zinaweza kupatikna kwa wazalishaji kadhaa kuungana na kuunda

umoja wao. Katika umoja huo wawakilishi wachache wanakuwa na jukumu la kutafuta

taarifa za masoko ya kuku sehemu mbali mbali ambako kunaweza kuwapa wazalishaji

tija zaidi.

Walio katika umoja huo watatumia taarifa hizo kufanya maamuzi ya kuuza kwa faida

zaidi kwa pamoja au kwa mmojammoja kutegemeana na hali halisi.

Previous Post Next Post