Kufuga ndani ya banda tu/ Intensive System

Kufuga ndani ya Banda tu
banda la kuku kienyeji
Njia nyingine ni kuwafuga kuku ndani tu. Katika njia hii, kuku hukaa ndani wakati wote.
Njia hii ya ufugaji utumiwa zaidi na wafugaji wa kuku wa kisasa. Lakini yaweza kutumika
hata kwa kuku wa asili hasa katika sehemu zenye ufinyu wa maeneo.
Changamoto/Hasara za ufugaji wa ndani ya banda tu
• Unatakiwa uwe na muda wa kutosha wa kuwahudumia kuku wako kikamilifu.
• Pia unatakiwa kuwa na mtaji mkubwa wa kujenga banda na kuwanunulia kuku chakula.
• Ugonjwa ukiingia na rahisi kuambukizana.

Vilevile kuku huweza kuanza tabia mbaya
kama kudonoana, n.k.
Faida za kufuga ndani tu
• Ni rahisi kutambua na kudhibiti magonjwa.
• Ni rahisi kudhibiti upotevu wa kuku, mayai na vifaranga.
• Ni rahisi kuwapatia chakula kulingana na mahitaji ya kila kundi.
• Ni rahisi kuwatambua na kuwaondoa kuku wasiozalisha katika kundi.


...........................................................................................................................................
Previous Post Next Post