Kufuga kuku nusu huria

Image result for banda la kuku kienyejiKufuga nusu ndani – nusu nje
Huu ni mtindo wa kufuga ambapo kuku wanakuwa
na banda lililounganishwana uzio kwa upande
wa mbele. Hapa kuku wanaweza kushinda ndani
ya banda au nje ya banda wakiwa ndani ya uzio.
Ufugaji wa nusu ndani na nusu nje
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Wakati wa mchana kuku huwa huru kushinda ndani ya banda hasa wanapotaka kutaga
na wakati wa kuatamia au wanaweza kukaa ndani ya uzio nje.
Faida za kufuga nusu ndani na nusu nje
• Kuku wanakuwa salama mbali na maadui mbali mbali.
• Utaweza kuwalisha kuku wako vizuri hivyo wataweza kuongeza uzalishaji wa mayai
na wa nyama (kwa kukua haraka).
• Itakuwa rahisi kwako kudhibiti wadudu na vimelea vinavyoweza kuleta magonjwa kwa
kuku wako.
• Ni rahisi kuwatenganisha kuku katika makundi tofauti na kuwahudumia ipasavyo.
• Ni rahisi kutambua kuku wagonjwa kuliko kufuga huria.
• Kuku watapata mwanga wa jua wa kutosha pamoja na hewa safi.Wakati wa jua kali
watakuwa huru kuingia ndani ya banda na kukaa kivulini.
• Kuku hawatafanya huharibifu wa mazao yako shambani au bustanini na kwa majirani
zako.
• Utapata urahisi wa kukusanya na kupeleka mbolea bustanini au shambani.
Changamoto/Hasara ya kufuga nusu ndani na nusu nje
• Huna budi uwe na muda wa kutosha kwa ajili ya kuwahudumia kuku wako.
• Pia utahitaji kuwa na eneo kubwa kiasi la kufugia.
• Pia utaingia gharama ya ziada kidogo ya kutengeneza banda na wigo na kuwapatia
uku chakula cha ziada.
• Hata hivyo gharama za muda huo na za vifaa vingine zitafidiwa na mapato ya ziada
utakayopata kwa kufuga kwa njia hii.

 .....................................................................................................................
Previous Post Next Post