Ufugaji bora wa sungura

https://www.animalscience.care/
Ufugaji bora wa sungura
UFUGAJI WA NJE
1. Sehemu yote izungushiwe wavu  kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk
2. Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
3. Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4. Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng'oa yote)


MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku.


CHAKULA
Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates).


USAFI
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto.

DAWA
Hakikisha wanapata dawa za minyoo  kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powder zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto,

MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, zingatia manyoya hayanyonyoki,kama yakinyonyoka ni tatizo

Kumbuka:usithubutu kuwapa dawa nyingine bila ushauri wa kitaalam,Antibiotics usijaribu kuwapa.


......................................................................................................................................
Previous Post Next Post