UFUGAJI BORA WA NG'OMBE WA MAZIWA

https://www.animalscience.care/
Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi,mbolea na hutumika kama wangyama kazi.  Zaidi ya asilimia95 ya ng,ombe na hutumika kama wanyama kazi.  Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa asili ambao huzalisha nyama na maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na wale wachache walioboreshwa.  Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili, wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama na wanaofugwa kwa ajili ya maziwa. 

Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa na ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na:
  • Kufuga ng’ombe katika eneo kwa kuzingatia uwianao wa idadi ya ng’ombe na malisho katika mfumo wa ufugaji huria.
  • Kujenga banda au zizi bora.
  • Kuchagua koo/aina ya ng’ombe kulingana na uzalishaji (nyama au maziwa).
  • Kutunza makundi  mbalimbali ya ng’ombe kulinga na umri na hatua ya uzalishaji.
  • Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili.
  • Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifguo.
  • Kuvuna mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana na mahitaji ya soko.
  • Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi zinazokidhi viwango vya ubora na usalama.
  • Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu ya ufugaji.


MIFUMO YA UFUGAJI
Ng’ombe wanaweza kufugwa katika mfumo wa ufugaji huria au kulishwa katika banda (ufugaji shadidi).  Ufugaji huria huhitaji eneo kubwa la ardhi yenye malisho mazuri na vyanzo vya maji.  Pamoja na kuwa na ufugaji huu, ni muhimu ardhi hiyo itunzwe kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho.  Ufugaji wa shadidi uzingatie uwepo wa banda bora na lishe sahihi.

UFUGAJI KATIKA MFUMO HURIA
Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora katika ufugaji huria anapaswa kuzingatia yafuatayo:-

  • Atenge eneo la kutosha la kufugia kulingana na idadi ya ng’ombe alionao.
  • Atunze malisho ili yawe endelevu na yapatikana wakati wote.
  • Awe na eneo lenye maji ya kutosha na
  • Atenganishe madume na majike ili kuzuia ng’ombe kuzaa bila mpangilio.

Matunzo mengine ya ng’ombe yazingatie vigezo vingine muhimu kama umri hatua ya uzalishaji na matumizi ya ng’ombe husika.

................................................................................................
Previous Post Next Post