Utunzaji wa Vifaranga
Malezi bora ya vifaranga ni
muhimu katika ufugaji wa kuku kwa sababu
vifaranga hawana uwezo wa
kustahimili mazingira wakiwa wenyewe mara
wanapoanguliwa.Ukosefu wa
malezi bora husababisha vifaranga kuwa
dhaifu,kufa kwa wingi na hivyo
kupunguza idadi ya kuku wa baadaye.
Malezi ya vifaranga yanaweza
kufanyika kwa kutumia kuku walezi au
kutumia vifaa maalum.
Kulea
Vifaranga kwa Kutumia Kuku Mlezi
Vifaranga wanaweza kulelewa na
mama yao au kuku mlezi. Endapo kuku
wengi wametotoa vifaranga kwa
wakati mmoja, achaguliwe kuku mlezi
aliye na uwezo wa kulea
vifaranga wengi kati ya waliototoa aendelee kulea
na wengine waliototoa waachwe
huru ili warudi kwenye mzunguko wa
kutaga. Kuku mmoja anaweza
kulea vifaranga 20 hadi 25. Mfugaji wa
kuku,pamoja na kanuni
nyingine, anapaswa kuzingatia yafuatayo:-
Kuku
anayelea vifaranga atengewe chumba maalumu, apewe maji ya
kutosha na chakula chenye
virutubisho muhimu,
Vifaranga
wasiachiwe kutoka nje hadi watakapofika umri wa wiki 6,
Vifaranga
watengwe na mama/mlezi baada ya wiki 4 kuruhusu mama
aendelee na mzunguko wa
kutaga;na
Katika
maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi vifaranga
wacheleweshwe kutenganishwa na
mama/mlezi hadi wiki ya 6 au
mpaka waonekane wameota
manyoya ya kutosha
Kulea
Vifaranga kwa Kutumia Bruda
Bruda ni chombo/sehemu
iliyoandaliwa mahusus kwa ajili ya kuwapatia
joto vifaranga badala ya
mama/mlezi. Mfugaji anaweza kulea vifaranga
wengi kwa kutumia bruda ambayo
ni mduara unaweza kutengenezwa kwa
kutumia mbao, karatasi ngumu
au kwa kuziba pembe za chumba.Aidha,
njia hii hupunguza vifo vya
vifaranga vinavyosababishwa na ndege au
wanyama hatari,huruhusu kuku
kutaga mapema zaidi na kuwa na
mizunguko mingi ya utagaji
(kwa kuku wanaoatamia). Vilevile, hurahisisha
udhibiti wa magonjwa.
Mfugaji
anapaswa kufuata taratibu zifuatazo katika kulea vifaranga kwa
kutumia
bruda:-
Kuweka
vifaa vya kuongeza joto kwa mfano taa ya umeme, chemli au
jiko la mkaa. Zingatia kiwango
cha joto kinachohitajika katika bruda.
Wiki ya kwanza ni 35oc,
wiki ya pili ni 33oc, wiki ya tatu ni 31oc na
wiki ya nne ni 29oc,
Kuchunguza
mtawanyiko wa vifaranga ndani ya bruda ili kutathimini
hali ya joto.Wakijikusanya
kwenye chanzo cha joto, inaashiria kuwa
baridi imezidi hivyo joto
liongezwe. Wakiwa mbali na chanzo cha joto
maana yake joto limezidi hivyo
joto lipunguzwe,
Bruda
iwe na sakafu yenye malalo yatokanayo na maranda ya mbao
au pumba za mpunga. Malalo
yabadilishwe endapo yataonekana
yameloana,
Bruda
iwekwe vifaa vya maji na chakula. Maji na chakula kiwekwe
kabla ya kuweka vifaranga,
Vifaa
vya joto viwekwe ndani ya bruda masaa 6 kabla ya kuingiza
vifaranga,
Vifaranga
walishwe chakula cha kuanzia gramu 12-15 kwa kipindi
cha wiki ya 2. Katika wiki ya
3 wapewe gramu 21-35 kwa kifaranga
na chakula hicho kiwepo muda
wote,
Vifaranga
wapatiwe vitamin, madini na dawa za kinga (antibiotics); na
Vifaranga
wapatiwe chanjo kulingana na maelekezo ya mtaalamu wa
mifugo.Chanjo dhidi ya
magonjwa muhimu kwa mfano,Marek’s (mara
anapototolewa), Mdondo (siku
ya 3-4 na kurudiwa baada ya siku ya
21 na kila baada ya miezi 3)
na Gumboro (siku ya 7na kurudia tena
siku ya 21).Wapatiwa dawa ya
minyoo (wiki ya 8) na coccidiosis(wiki
ya 3-4). Siku ya 45 wapewe
chanjo ya ndui ya kuku.
2. Kutunza Kuku Wanaokua (Wiki 8-18)
Utunzaji
wa kundi hili unategemea mfumo unaotumika.
Kuku Wanaofugwa Katika Mfumo
Huria
Kuku wanaofugwa katika mfumo
huu wapatiwe matunzo bora
yakiwemo yafuatayo;
ü Wapewe
chakula cha ziada asubuhi kabla ya kutoka na
wanaporudi
kwenye banda. Chakula hicho kinaweza kugawanywa
mara
ya 2 kwa siku,
ü Wapatiwe maji safi na
ya kutosha wakati wote
ü Wapatiwe chanjo na dawa
kulingana na ushauri wa mtaalam wa
mifugo.
Wiki ya kumi warudie chanjo ya mdondo, wiki ya 12
kuhara
(fowl cholera), wiki ya 14 ndui ya kuku,
Kuku
Wanaofugwa Katika Mfumo Shadidi
Majogoo watenganishwe na
mitetea katika wiki 7 hadi 10 ili
kuzuia uzaliano usio na
mpangilio,
Wapewe chakula cha kukuzia
kuanzia wiki ya 8-15 gramu 55-
60 na kuanzia wiki ya 16 gramu
65-80 kwa wanaofugwa mfumo
huria na gram 120-125 kwa kuku
kwa siku kwa wanaofugwa
mfumo wa shadidi,
Kuku wa nyama wapatiwe chakula
cha kuku wa nyama muda
wote,
Wapatiwe maji safi ya kunywa
kwa muda wote kwenye
vyombo safi,
Kuku wachunguzwe dalili zozote
za ugonjwa ili waweze kupata
tiba sahihi kutoka kwa
mtalaamu wa mifugo,
Kuku wa wiki 9-20 wanahitaji
nafasi ya mita za mraba 0.15 kwa
kuku na wiki 21 au zaidi mita
za mraba 0.2 kwa kuku,
Kuwe na vyombo maalum vya
kutosha kwa ajili ya chakula na
maji,
Wafanyiwe usafi wa banda mara
kwa mara ili kuzuia magonjwa
yanayotokana na uchafu
Wakatwe midomo ili kuzuia
kudonoana.
Kuku Wanaotaga
Mahitaji ya kuku wanaotaga ni
tofauti na makundi mengine.
Mambo
ya kuzingatia kwa kuku wanaotaga ni pamoja na:-
1.
Banda liwe na viota vya
kutagia mayai (kiota 1 kwa kuku 3-
2.
Viota viwekwe bandani mara kuku watakapofikisha
umri wa
wiki
18 ili waanze kuzoea kuvitumia,
3.
Wapatiwe chakula na maji safi
wakati wote kwa kutumia
vyombo
maalum ambavyo ni visafi,
4.
Kuku wasiotaga waondolewe
kwenye kundi.Kuku hao
huonekana
wasafi na sehemu ya kutolea yai huwa ndogo na
kavu,upanga
wake kichwa (comb) huwa mdogo na
mwekundu,
5.
Wapatiwe dawa ya minyoo kila
baada ya miezi 3,
6.
Wawekewe fito au ubao
mwembamba kama sehemu ya
kupumzikia
na mazoezi ili kuzuia kudonoana,
7.
Mayai yakusanywe mara 4 au
zaidi kwa siku ili yasidonolewe
na
kuku,
8.
Kuwe na malalo makavu na
yabadilishwe mara yanapochafuka,
9.
Vyombo vifanyiwe usafi kila
ili kuzuia magonjwa; na 10.Watundikiwe
majani mabichi aina ya mchicha,papai,
alfaafa au majani jamii
ya mikunde .......................................................................................
Tags:
UFUGAJI KUKU
