Sasa


Fahamu chakula na uzalishaji nguruwe


https://www.animalscience.care/
CHAKULA NAUZALISHAJI WA NGURUWE
Chakula cha nguruwe ni muhimu kiandaliwe kulingana ma
umri wa nguruwe

Matumbo ya nguruwe hayana tofauti sana na matumbo
ya binadamu wana tumbo moja ambao hivyo nguruwe wanakula chakula cha nafaka
 mahindi
,ngano na
mihogo,pia vyakula vya mizizi
·       nyama,
·       maboga
·       ,samaki,
·       mashudu na pumba
Na zaidi yahapo maji ni lazima nguruwe wapatiwe
 Mazao hayo yotepamoja na chumvi,unga wa mifupa,huleta mchanganyiko mzuri kufuatana na mahitaji ya mfugaji wa
nguruwe na nguruwe mwenyewe kufuatana na
umri&madhumuni,hivyo basi
mchanganyiko huo ni lazima huwe na mambo muhimu
yafuatayo protini,nishati,mafuta,vitamin,madini,maji ni kitu cha lazima.
 PROTINI
Protini ni sehemu ya chakula ambayo ni muhimu sana
katika kujenga mwili au nyama ya kila nguruwe na kila
mnyama,protini ni sehemu kama mkanda uliotengenezwa
kwa kuunganisha sehemu ndogo sana ziitwazo amino
acids
vyakula venye asili ya protini ni
Samaki,mashudu,ufuta,,damu ya wanyama iliyo kaushwa.
NISHATI/KABIHAIDRETI (wanga,sukari na nyuzi nyuzi(fibre)
Umuhimu wa kabohaidreti katika mwili ni
•Huleta nguvu mwilini
•Husaidia kutengeneza maziwa,
Vyakula viletavyo nguvu mwilini kwa wingi ni
·       Mahindi
·       mtama,
·       Mihogo
·       na pumba
MAFUTA
Matumizi ya mafuta katika mwili wa nguruwe
• Mafuta huleta nishati ya mwili kwa wingi sana.
• Mafuta husaidia joto kupotea katika mwili.
• Mafuta huyeyusha vitamin A,D&E
VITAMINI NA MADINI
Madini yanahitajika kwa wingi kama calcium na
phosphorus chakula cha kulisha nguruwe wa
kunenepesha
Chumvi ikiwa nyingi sana katika chakula humfanya
nguruwe anywe maji mengi sana na hatimaye kuharisha
sana matokeo yake ni hukua polepole na wanyama hao
hula chakula kingi sana za kuongeza kilo moja ya nyama.
MAJI
Maji ni muhimu sana katika mwili wa nguruwe,
huyeyusha chakula tumboni,kusafirisha damu na mkojo,
pia hurekebisha joto katika mwili wa nguruwe.
Kama maji
yatakosekana,
•Mnyama hudumaa sana.
•Utoaji wa maziwa ni mdogo sana
• Uzito wa mnyama hupungua na uzito huo ukipungua
kwa asilimia 10 mnyama huugua na ikiwa chini ya
asilimia 25 mnyama anaweza kufa.
MAHITAJI YA MAJI KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE
Eneo la ufugaji nguruwe huitaji kuwa na chanzo cha maji
safi kwjili ya kunywa na usafi wa mabanda.
Nguruwe aliyekomaa huitaji walau lita 6 za maji kila siku,
na nguruwe anayenyonyesha lita 12
Mahitaji ya maji ya kunywa kwa kila nguruwe ni kam
ifuatavyo
• Nguruwe anayenyonyesha lita 20 kwa siku
• Nguruwe aliyeachishwa kunyonyesha lita 5 kwa siku,
Nguruwe wanaokuzwa na kunenepesha kilo 20 - 90 lita 5
kila siku.
• Watoto wa nguruwe lita 1 kila mmoja.

....................................................................................................................................
Previous Post Next Post