Kuna usemi usemao "mali bila daftari hupotea bila
habari" ukiwa na mradi wowote wa ufugaji ni vema ukiwa unaweka kumbukumbu
za kila siku au kwa kila wiki. Katika kutunza kumbukumbu za ufugaji kuna mambo
muhimu ya kuyazingatia kama ifuatavyo:-
1. KUMBUKUMBU ZA KUKU NA UZALISHAJI
Hii ni kuanzia unapowapokea hadi
kuwatoa bandani. Hapa unapaswa kila siku uwaangalie kuku wako ili kujua
wanahali gani na ni wangapi waliopo, hapo utaelewa kama kuna ugonjwa wa kutibu
au tahadhari gani zichukuliwe.
kama ni kuku wa mayai basi kujua idadi ya mayai wanyotaga
kila siku, ili uweze kujua asilimia za utagaji na uweze kupima kiwango chao cha
utagaji.
2. KUMBUKUMBU ZACHANJO
Weka kumbukumbu za chanjo dhidi ya
magonjwa mbalimbali kama vile mdondo (Newcastle), gumboro, ndui na magonjwa
mengine.
3. KUMBUKUMBU ZA
AFYAHapa unarekodi kila aina ya ugonjwa uliotekea bandani, idadi ya
walioathirika, waliotibiwa, waliopona na waliokufa. Gharama za matibabu nazo
pia ziwekwe kwenye kumbukumbu.
4. GHARAMA ZA VIFAA NA CHAKULAVifaa vyote unavyonunua kwa
ajili ya ufugaji ni lazima viorodheshwe na viwekwe kwenye kumbukumbu, na gharama
za chakula kuanzia unapoingiza kuku hadi unapowatoa iwekwe kwenye kumbukumbu
pia.
MUHIMU:
Njia rahisi ya kutunza kumbukumbu ni kununua daftari
na kutengeneza majedwali yanayoonesha vipengele tajwa hapo juu.
.............................................................................................................................
.............................................................................................................................
Tags:
MBINU ZA UFUGAJI
