AINA ZA CHAKULA NA MFUMO WA KULISHA:
KUKU WA NYAMA(broilers)
Broiler finisher hadi kuuza.
UTARATIBU WA CHANJO
Umri wa siku 7:
Newcastle(kideri)
Umri wa siku14 :
Gumboro
Umri wa siku 21: New
castle(kideri)
Umri wa siku
28:Gumboro
Sifa za banda bora la kuku..
1. Liwe limejengwa mahali palipokingwa na upepo mkali.
2. Liwe na mwanga wa kutosha.
3. Madirisha yaruhusu hewa safi kuingia na chafu kutoka
(Cross Ventilation).
4. Sakafu isiruhusu maji kutuama wala maeneo yanayozunguka
banda.
5. Paa lisiruhusu mvua kuingia.
6. Banda liwe linasafishika kwa urahisi na kuta imara.
7. Banda liwe na nafasi ya kutosha kwa ajili ya kuku, vyombo
vya maji na chakula,
NAFASI YA KUKU WA NYAMA (STOKING RATE)
Mita za mraba (m2): 4m2=kuku 50-100
MATATIZO YALETWAYO NA UPUNGUFU WA VITAMINI MWILINI(2)
VITAMINID
Husaidia madini aina ya calcium na phosphorous kuchukuliwa
na mwili ili kuimarisha mifupa na kutengeneza ganda la yai la kuku. Jua
husaidia mwili wa kuku kutengeneza vitamini D.
Dalili za Upungufu wa Vitamini D Mwilini
Rickets: Mifupa huwa laini(soft), hupinda, magoti huvimba,
na midomo huwa laini. Hii hutokana na madini aina ya calcium na phosphorous
kutojengeka kwenye mifupa.
Kukua polepole.
Uanguaji hafifu wa mayai.
VITAMINIE
Dalili za Upungufu wa Vitamini E Mwilini
Ugonjwa uitwao "crazy chick" au "nutritional
encephalomalacia" ambapo ubongo wa kuku huwa laini na kuathiri mishipa ya
fahamu.
Dalili zake ni
-Shingo hupinda
-Kifaranga huanguka kifudifudi
-Kichaa
VITAMINI K
Husaidia kuzuia kuvuja damu. Ikikosekana mwilini mishipa ya
damu hupasuka na kusababisha damu kuvuja. Vitamini hii hupatikana katika
alfalfa, samaki (fish meal) na nyama.
VITAMINI B1 (THIAMIN)
Huleta hamu ya kula.
Upungufu hufanya kichwa kurudi nyuma (Head retraction)
Siyo rahisi kupata
upungufu wa vitamini B1 mwilini kwa kuwa vyakula vingi vina vitamini
hii.Hupatikana katika nafaka, alfalfa na mafuta (oil).
NAMNA YA KUZUIYA MAGONJWA
Weka dawa ya kuua wadudu kwenye chimbo mlangoni ili watu
waikanyage
(disinifectant +maji)
Punguza mwanga kwa kuku wanaokua
Wiki ya kwanza tumia dawa aina ya ANTIBIOTIC na VITAMIN
kwenye maji
hapa ni vizuri ukapata ushauri
...........................................................................................................................................
...........................................................................................................................................
Tags:
UTOAJI CHANJO
