Njia za ufugaji kuku huria I Mshindo media

Image result for banda la kuku kienyejiNjia tofauti za kufuga kuku


Njia za ufugaji kuku
Mambo yanayomfanya mfugaji kuamua atumie njia fulani ya kufuga ni pamoja na uwezo
wa kugharamia shughuli ya ufugaji wa kuku na ukubwa wa eneo alilonalo la kufugia.
Katika sehemu hii utajifunza njia tatu za kufuga kuku ambazo ni:
1. Kufuga huria
Kuku huachwa wenyewe kujitafutia chakula na
maji. Njia hii inatumika zaidi kufuga kuku wa
kienyeji.
 Mara chache sana mfugaji huwapatia
kuku chakula cha ziada. Kwa ufugaji huu lazima
kuwe na eneo kubwa la kutosha kuku kuzunguka
na kutafuta chakula. Kuku hulala eneo lisilo rasmi
kama vile jikoni, kwenye kiambata n.k.
Faida zake
• Ni njia rahisi ya kufuga.
• Gharama yake pia ni ndogo.
• Kuku wanapata mazoezi ya kutosha.
• Kuku wanapata chakula mchanganyiko ambacho kinafaa kiafya.
Hasara zake
• Kuku huwa hatarini kuibiwa au kudhurika na wanyama wakali na hali mbaya ya hewa.
• Ukuaji wa kuku ni hafifu, hufikia uzito wa kilo 1.2 baada ya mwaka.
• Huharibu mazingira kama kula na mimea ya  bustanini mazao kama nafaka.
• Ni rahisi kuambukizwa magonjwa.

......................................................................................................................................
Previous Post Next Post