Chakula
kikuu cha ng’ombe ni nyasi na majani jamii ya mikunde ambayo haia madhara kwa afya
ya mnya
Malisho ya Asili
Malisho
haya kwa kawaida hukua haraka na kupoteza viinilishe muhimu, kwa muda mfupi
baada
ya mvua. Malisho ya asili huwa na viinilishe vinavyotosheleza mahitaji ya
mifugo na
wakati
wa kiangazi malisho huwa duni na yasiyotosheleza. Wakati malisho yanatosheleza
ng’ombe
huwa na uzito wa kuridhisha tofauti na wakati wa kiangazi ambapo ng’ombe
hupungua
uzito. Malisho ya asili ya jamii ya nyasi huwa na upungufu wa viinilishe
hususani
protini.
Mikunde ina tabia yakutopungua viinilishe haraka ikilinganishwa na nyasi.
Malisho yaliyoboreshwa
Malisho
ya asili yanaweza kuboreshwa kwa kuongeza mimea aina ya mikunde, kuongeza
nyasi
bora kwenye malisho, kuongeza samadi kwenye mbuga za malisho. Malisho
yaliyoboreshwa
yana uwezo wa kuwafanya wanyama wakue haraka na kufikia uzito wa
kuchinjwa
mapema.
Taratibu za kuboresha malisho/ Mambo ya kuzingatia
i.
Uwezo wa kuvumilia hali ya hewa na mazingira yaliyopo
ii.
Yawe yenye kuvumilia magonjwa na wadudu waharibifu
iii.
Yawe yasiyozidiwa nguvu na magugu
iv.
Yawe yenye kustahimili kuchungwa
Inafaa
maeneo ya kuchungia/kulishia yatengwe na kugawanywa katika sehemu ambazo
nyasi
zitaoteshwa na kukuzwa. Hatimaye nyasi hizo zichungwe kwa nyakati tofauti ili
kuepuka
uharibifu na kuhakikisha kuwa nyasi zinatosheleza vipindi vyote vya mwaka.
Utaratibu
huo utasaidia pia kupunguza uwezekano wa mifugo kuambukiza magonjwa.
Uhifadhi wa malisho
Malisho
hupatikana kwa wingi wakati wa masika, na wakati huo yana ubora unaotakiwa.
Wakati
wa masika, mifugo hula malisho na kusaza ambapo wakati wa kiangazi malisho
huwa
haba na virutubisho hupungua ili kuwa na uhakika na upatikanaji na chakula cha
kutosha
na bora wakati wote, ni muhimu kuhifadhi malisho ya ziada katika kipindi hicho.
Njia za kuhifadhi malisho
Kuna
njia kuu mbili za kuhifadhi malisho nazo ni;
i.
Kuyakausha (Hei)
ii.
Kuyavundika (Saileji)
Kuyakausha (Hei)
Hei
ni majani makavu ambayo yanaweza kulishwa wanyama yangali shambani au kuvunwa
na
kufungwa kwenye marobota kisha kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadae
Hatua ya kutayarisha
i.
Vuna majani yanapoanza kutoa maua
ii.
Yaanike na yageuze majani mara moja au mara mbili kwa siku ili yakauke vizuri
iii.
Ukaushaji huchukua siku tatu hadi sita kutegemea aina ya majani au hali ya hewa
iv.
Majani yakiisha kauka yafunge kwenye marobota
v.
Yahifadhi marobota sehemu isiyoingiza mvua au unyevu
vi.
Marobota ya majani makavu yanaweza kutengenezwa kwa mashine au kwa
kutumia
makasha ya mbao.
vii.
Mfugaji mdogo anashauriwa kutumia makasha ya mbao kwa kutengeneza
marobota
hayo.
viii.
Makasha ya mbao yanaweza kutengenezwa kwa kutumia vipimo vifuatavyo,urefu
sentimita
75, upana sentimita 45 na kina sentimita 35.
ix.
Majani yaliyofungwa katika marobota hutumia sehemu ndogo ya kuhifadhia na pia
hupunguza
upotevu.
x.
Mfugaji anaweza kukadiria kiasi cha malisho atakayotumia kulisha ng’ombe wake
kwa
msimu wa kiangazi.
Masalia ya mazao
shambani
Masalia
ya mazao kutoka shambani yanaweza kutumiwa ili kufidia chakula ambacho
ng’ombe
amekikosa kutokana na uhaba wa majani wakati wa kiangazi. Masalia yanaweza
kuwa
ya mabua ya nafaka mbalimbali kama vile mahindi, mtama, mpunga, ulezi, ngano au
uwele.
Mengine ni majani ya viazi vitamu, miwa au majani ya jamii ya mikunde kama vile
maharage,kunde,
njugu mawe au mbaazi.
Masalia
yanaweza kutumiwa na ng’ombe moja kwa moja bila kuboreshwa. Hata hivyo
ng’ombe
hawezi kula kwa wingi na hivyo inashauriwa kuyanyunyuzia molasses au magadi
ili
ng’ombe aweze kula mengi zaidi.
Maji
Maji
ni muhimu katika kupoza joto la mwili kutengeneza maziwa, kusafirisha
virutubisho
na
kutoa uchafu mwilini kwa njia ya mkojo,kinyesi kupumua na jasho. Ng’ombe
akipata
maji
ya kutosha hukua vizuri, huwa mwenye afya na hutoa maziwa mengi na bora. Kiasi
cha
asilimia 85 hadi 87 ya maziwa ni maji. Ng’ombe anapokosa maji hukosa hamu ya
kula
na
hali hiyo ikiendelea hupungukiwa maji na hupoteza uzito. Ng’ombe anaweza kupata
maji
kwa njia zifuatazo;
i.
Kunywa
ii.
Kula vyakula vyenye maji maji
Vyakula vya ziada
Hakikisha
mifugo yako wanapata vyakula vya ziada kama vile
i.
Pumba za mahindi, mtama,ngano
ii.
Mashudu ya pamba au alizeti
16
iii.
Madini
iv.
Vitamini
Unenepeshaji wa ng’ombe wa asili kwa ajili ya soko
Umri
unaofaa kumuuza ng’ombe wa asili ili kupata nyama bora ni miaka mitatu na nusu.
Katika
umri huu ng’ombe wanaotegemewa kupelekwa kwenye soko kwa ajili ya
kuchinjwa
ni madume, maksai na mitamba wasiofaa kuzaai. Ili kupata bei nzuri ya
ng’ombe
mfugaji anatakiwa kuzingatia ubora wa mifugo yake kulingana na madaraja. Hapa
nchini
ng’ombe wa nyama wanaouzwa wameainishwa katika madaraja matano ambayo ni:
i.
Tanzania bora
ii.
Daraja la kwanza
iii.
Daraja la pili
iv.
Daraja la tatu
Tags:
MBINU ZA UFUGAJI
