UFUGAJI
NG’OMBE WA KIENYEJI
Ufugaji
wa ng’ombe wa Asili hufanyika katika mashamba makubwa ya serikali, mashamba
madogo
na wafugaji wadogo.
Ng’ombe wa maziwa wa asili hufugwa kwa wingi
katika
mikoa
ya Kagera, Arusha, Mbeya, Manyara na Kilimanjaro. Hata hivyo, wanaweza
kupatikana
pia katika mikoa ya Iringa, Dar es Salaam, Morogoro na Iringa. Ufugaji bora
wa
ng’ombe wa maziwa humuongezea kipato mfugaji pamoja na kujipatia lishe
itokanayo
na
maziwa.
Ufugaji
holela wa ng’ombe ni ule usiozingatia kanuni na misingi ya ufugaji na una
madhara
makubwa.
Madhara
hayo ni pamoja na:
- Kupata mapato duni
- Uharibifu wa mazingira
- Ugonvi na migogoro katika jamii.
- Kutumia muda mwingi katika kuchunga badala ya shughuli nyingine
- Ni rahisi ng’ombe kushambuliwa na kueneza magonjwa
- Watoto hukosa elimu kwa kuwa hujihusisha na kuchunga ng’ombe
- Malisho duni kutokana na kufunga ng’ombe kuliko uwezo wa nyanda husika
- Ufugaji huu hauzingatii ubora bali wingi wa mifugo.
Sifa za ng’ombe wa
asili
i.
Wana uwezo wa kustahimili magonjwa
ii.
Hustahimili muda mrefu bila malisho yakutosha
iii.
Wanaweza kutembea mwendo mrefu kutafuta maji na malisho
iv.
Nyama na maziwa yao yana ladha nzuri
Tags:
MBINU ZA UFUGAJI