KUJUA AFYA YA KUKU



kuku

KUJUA KUKU MGONJWA NA MWENYE AFYA
Ugonjwa ni nini? Ugonjwa ni mabadiliko kutoka katika afya ya kawaida ya mnyama/kuku. Hali hii hutokea pale
vimelea au vijidudu vinapoingia mwili wa mnyama, kwa kula vyakula vyenye sumu, au inapotokea kuna uhaba walishe au madini mwilini.
Kuku mwenye afya nzuri

N
Kuku asiye na afya nzuri (mgonjwa)

Macho na sura angavu
Hupenda kula na kunywa maji
Pua zilizo safi, upanga na undu mwekundu, manyoya
laini na yaliyopangika vizuri
Hupumua kwa utulivu
Sehemu ya kutolea haja huwa kavu
Kinyesi kikavu, cheupe na kisicho na rangi
Hutaga mayai kawaida

Huonekana mchovu na dhaifu
Hula na kunywa kidogo au zaidi ya kawaida
Hutoa kamasi puani, ute na matongotongo;
 manyoya
yaliyovurugika
Hupumua kwa shida na kwa sauti
Sehemu ya kutolea haja inakuwa na unyevunyevu na
kinyesi kuganda
Huharisha, kinyesi huwa na damu au minyoo
Hutaga mayai machache au husimama kutaga kabisa
Huwa na tabia ya kujitenga na wenzake katika kundi

Previous Post Next Post