KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA NG’OMBE WA MAZIWA PAMOJA NA
NGURUWE.
(UFUGAJI WA NDANI-ZERO
GRAZING)
Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya maziwa .Hawa ni wale wachache walioboreshwa. Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili, wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama na wanaofugwa kwa ajili ya maziwa. Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya maziwa mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na:-
i) Kufuga
ng’ombe katika zizi/banda kwa kuzingatia uwianao wa idadi ya ng’ombe
ii) Kujenga
banda au zizi bora.
iii)Kuchagua
koo/aina ya ng’ombe kulingana na uzalishaji maziwa.
iv) Kutunza
makundi mbalimbali ya ng’ombe kulinga na umri na hatua ya
uzalishaji.
v) Kumpa
ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili.
vi) Kudhibiti
magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifguo.
vii)Kuvuna
mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana na mahitaji ya soko.
viii)Kuzalisha
maziwa yanayokidhi viwango vya ubora na usalama.
ix)Kutunza
kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu ya ufugaji.
MIFUMO YA UFUGAJ
Ng’ombe wanaweza kufugwa katika
mfumo wa ufugaji huria au kulishwa katika banda (ufugaji
shadidi). Ufugaji huria huhitaji eneo kubwa la ardhi yenye malisho
mazuri na vyanzo vya maji. Pamoja na kuwa na ufugaji huu, ni muhimu
ardhi hiyo itunzwe kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho. Ufugaji
wa shadidi uzingatie uwepo wa banda bora na lishe sahihi.
UFUGAJI KATIKA MFUMO HURIA
Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi
na bora katika ufugaji huria anapaswa kuzingatia yafuatayo:-
- Atenge
eneo la kutosha la kufugia kulingana na idadi ya ng’ombe alionao.
-Atunze
malisho ili yawe endelevu na yapatikane wakati wote.
-Awe
na eneo lenye maji ya kutosha
-Atenganishe
madume na majike ili kuzuia ng’ombe kuzaa bila mpangilio.
Matunzo mengine ya ng’ombe
yazingatie vigezo vingine muhimu kama umri hatua ya uzalishaji na matumizi ya
ng’ombe husika.
BANDA/ZIZI BORA LA NG’OMBE
BANDA BORA.
Band lijengwe sehemu ya mwinuko
mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-
ü Uwezo wa kumkinga ng’ombe dhidi ya mvua, upepo, jua kali na
baridi.
ü Kuta imara zenye matundu au madirisha kwa ajili ya kuingiza
hewa na mwanga wa kutosha,
ü Sakafu yenye mwinuko upande mmoja ili isiruhusu maji na
uchafu kutuama.
ü Lijengwe katika hali ya kuruhusu kufanyiwa usafi kwa urahisi
kila siku, na sakafu ngumu ya zege au udongo ulioshindiliwa na kuweka malalo.
ü Paa lisilovuja.
ü Aidha kwa
wafugaji wanaofuga katika ufugaji huria ambako mazizi hutumika,
inashauriwa kuzingatia yafuatayo:-
ü Zizi likae mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama.
ü Zizi liweze kukinga mifugo dhidi ya wezi na wanyama hatari.
ü Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo ng’ombe
watengwe kulingana na umri wao.
ü Zizi lifanyiwe usafi mara kwa mara na
ü Liwe na sehemu ya kukamulia (kwa ng’ombe wa maziwa), stoo ya
vyakula, sehemu ya kutolea huduma za kinga na tiba(kibanio), eneo la kulishia
na maji ya kunywa.
ZIZI BORA
Zizi lijengwe sehemu ya mwinuko
isiyoruhusu maji kutuama mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa
zifuatazo:-
Liweze
kuhakikisha usalama wa ng’ombe.
Ukubwa
wa zizi uzingatie idadi ya mifugo.
Liwe
na sakafu ya udongo ulioshindiliwa vizuri na kufanyiwa usafi mara
kwa mara
Zizi
la ndama liwe na paa imara
Lijengwe
kwa vifaa madhubuti na visivyoharibu ngozi.
NG’OMBE WA MAZIWA.
Sifa za ng’ombe wa maziwa:-
- Umbo
lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea kichwani.
- Mgongo
ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani
- Miguu
ya nyuma mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele na
kwato imara.
- Kiwele
kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu na unene wa wastani
- Nafasi
kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha na
- Endapo
ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa kilichoshikamana vizuri mwilini, na
mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa.
Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa
kwa wingi nchini ni pamoja na Friesian, Ayrshire, jersey, Mpwapwa, Simmental na
chotara watokanao na mchangoayiko wa aina hizo na Zebu.
UTUNZAJI WA MAKUNDI MABALIMBALI YA
NG’OMBE WA MAZIWA KULINGANA NA UMRI NA HATUA YA UZALISHAJI
UTUNZAJI WA NDAMA
Mfugaji anapaswa kutunza ndama
vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi na bora kwa ajili ya
maziwa. Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama tangu
kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa ni pamoja na
- Kuhakikisha
kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia maambukizi ya viini ya magonjwa kupitia
kwenye kitovu, kwa mfano dawa joto (Tincute of Iodine) mara baada ya kuzaliwa
na
- Ndama
apatiwe maziwa ya awali yaani dang’a (colostrums) mara baada ya kuzaliwa kwa
lengo la kupata kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Aidha, aendelee
kunyonya maziwa hayo kwa muda wa siku 3-4.
Endapo jike aliyezaa amekufa au
hatoi maziwa, apewe dang’a toka kwa ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a
mbadala, ambayo inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo:-
- Lita
moja ya maziwa yaliyokamuliwa wakati huohuo.
- Lita
moja ya maji yaliyochemshwa na kupozwa hadi kufikia joto la mwili.
- Kijiko
kimoja cha chai cha mafuta ya samaki (cod liver oili).
-Mafuta
ya nyonyo vijiko vya chai 3 na
-Yai
moja bichi
Koroga mchanganyiko huo, weka katika
chupa safi na ndama anyweshwe kabla haujaopoa. Ndama anyweshwe
mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3 mfululizo na kila mara
mchanganyiko uwe mpya. Wakati wa kunywesha chupa iwekwe juu kidogo
ili asipaliwe.
- Endapo
ndama hawezi kunyonya ng’o mbe akamuliwe na ndama anyweshwe maziwa kwa njia ya
chupa kwa kuzingatia usafi wa maziwa na chupa.
-Ndama
aendelee kunyweshwa maziwa kwa kiasi kama ilivyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 1
-Ndama
aanze kuzoeshwa kula nyasi laini, pumba kidogo na maji safi wakti wote kuanzia
wiki ya 2 baada ya kuzaliwa na
- Ndama
aachishwe kunyonya au kupewa maziwa akiwa na umri wa miezi
3. Mfugaji ahakikishe kwamba ndama anayeachishwa kunyonya ana afya
nzuri.
JEDWALI NA. 1 KIASI CHA MAZIWA NA
CHAKULA MAALUMU KWA NDAMA
UMRI
(WIKI)
|
KIASI CHA
MAZIWA KWA SIKU (LITA)
|
KIASI CHA
CHAKULA MAALUM CHA NDAMA KWA SIKU (KILO)
|
1
|
3.0
|
0.0
|
2
|
3.5
|
0.0
|
3
|
4.0
|
0.0
|
4
|
4.5
|
0.0
|
5
|
5.0
|
0.1
|
6
|
5.0
|
0.2
|
7
|
5.0
|
0.3
|
8
|
4.0
|
0.4
|
9
|
3.0
|
0.7
|
10
|
2.0
|
1.0
|
11
|
1.5
|
1.25
|
12 – 16
|
0.75
|
1.5
|
Vyombo vinavyotumika kulishia ndama
visafishwe vizuri kwa maji yaliyochemshwa, sabuni na kukaushwa.
Matunzo mengine ya ndani ni pamoja
na:-
-Kuondoa
pembe kati ya siku 3 hadi 14 mara zinapojitokeza ili kuzuia wanyama kuumizana
na kuharibu ngozi,
-Kukata
chuchu za ziada kwa ndama jike
- Kuhasi
ndama dume wasiozidi umri wa miezi 3 ambao hawatahitajika kwa ajili kuendeleza
kizazi ili wakue haraka na kuwa na nyama nzuri.
-Kuweka
alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya tano, mfano
kuvalishwa hereni kwenye masikio kwa ajili ya urahisi wa udhiti wa umiliki na
utunzaji kumkukumbu na,
- Kuwapatia
kinga dhidi ya maabukizi na tiba ya magonjwa wanapougua.
UTUNZAJI WA NDAMA BAADA YA
KUACHISHWA MAZIWA HADI KUPEVUKA (MIEZI – 18)
- Ndama
baada ya kuachishwa maziwa apate malisho bora na chakula mchanganyiko kuanzia
kilo 2-4 kwa siku kutegemea umri wake na
- Ndama
wanapofikia umri wa miezi 18 wachaguliwe wanaofaa kuendeleza kizazi, wasio na
sifa nzuri waondolewe katika kundi.
UTUNZAJI WA MTAMBA
Mtamba ni ng’ombe jike aliyefikisha
umri wa kupandwa (wastani wa miezi 18) hadi anapozaa kwa mara ya
kwanza. Ni muhimu kutunza vizuri mtamba ili kupata kundi bora la
ng’ombe. Miezi 3 kabla ya kupandishwa mtamba apatiwe:-
-Malisho
bora
-Maji
ya kutosha
- Madini mchanganyiko
na
- Chakula
cha ziada kiasi cha kilo 2 – 3 kwa siku, ili kuchochea upevukaji na kuongeza
uzito wa mwili.
UTUNZAJI
WA NG’OMBE WAKUBWA
Kundi hili linajumuisha ng’ombe
wenye mimba, wanaokamuliwa na madume. Mfugaji anapaswa kutunza
vizuri ng’ombe wake wakubwa kwa lengo la kumpatia malisho bora na maji safi ya
kutosha kila siku. Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa
ng’ombe wakubwa ni pamoja na:-
- Ng’ombe
apatiwe majani makavu (hei) wastani wa kilo 10 au majani mabichi kilo 40 kwa
siku kutegemeana na uzito. Iwapo malisho hayatoshi hususan wakati wa
kiangazi apewe masalia ya mazao (viwandani na mashambani) kama molasisi, mabua,
maharage, mpunga n.k
- Ng’ombe
apewe vyakula vya ziada (pumba, mashudu, madini mchanganyiko, unga wa mifupa na
chokaa) kulingana na hatua na kiwango cha uzalishaji na
- Ng’ombe
apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
UPANDISHAJI
Mfugaji anapaswa kumpandisha ng’ombe
kwa umri na wakati muafaka ili kuepuka matatizo ya uzazi na pia kuhakikisha
anapata ndama bora na maziwa mengi. Mambo muhimu ya kuzingatia ni
pamoja na
- Mtamba
apandishwe akiwa na umri wa miezi 17 -24 na uzito wa kilo 230 – 300 kwa ng’ombe
wa kigeni na umri wa miezi 30 – 36 na uzito wa kilo 200 kwa ng’ombe wa
asili. (Rejea jedwali Na 2)
- Ng’ombe
aliyekwisha zaa apandishwe siku 60 baada ya kuzaa na
- Siku
18 – 23 baada ya kupandishwa, ng’ombe achunguzwe kama ana dalili za joto ili
apandishwe tena. Iwapo ng’ombe ataendelea kuonyesha dalili za joto
baada ya kupandishwa mara tatu mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo.
JEDWALI NA.2. UMRI NA
UZITO UNAOSHAURIWA KUPANDISHA MTAMBA
AINA YA
NG’OMBE
|
UZITO (KG)
|
UMRI
(MIEZI)
|
Friesian
|
240 – 300
|
18 – 24
|
Ayrshire
|
230 – 300
|
17 – 24
|
Jersey
|
200- 250
|
18 – 20
|
Mpwapwa
|
200 – 250
|
18 – 20
|
Chotara
|
230 – 250
|
18 – 24
|
Boran
|
200 – 250
|
24 - 36
|
Zebu
|
200
|
30 -36
|
DALILI
ZA NG’OMBE ANAYEHITAJI KUPANDWA
Ni muhimu mfugaji akazitambua dalili
za ng’ombe anayehitaji kupandwa ili aweze kumpandisha kwa
wakati. Dalili hizo ni pamoja na
Kupiga kelele mara kwa
mara
Kutotulia/kuhangaika
Kutokwa na ute mweupe
usiokatika ukeni
Kupenda kupanda wenzake
na husimama akipandwa na wenzake na
Kunusanusa ng’ombe
wengine
Ng’ombe akionyesha dalili za joto
apandishwe baada ya masaa 12, kwa kuhimilisha au kwa kutumia dume bora (kwa
mfano, akionyesha dalili asubuhi apandishwe jioni na akionyesha dalili jioni
apandishwe asubuhi).
KUMBUKA; Ng’ombe
aliyepandishwa apimwe mimba siku 60 hadi 90 baada ya kupandishwa.
MATUNZO YA NG’OMBE MWENYE MIMBA
Ng’ombe mwenye mimba huchukua miezi
9 hadi kuzaa. Katika kipindi hicho chote anastahili kupatiwa lishe
bora na maji ya kutosha ili akidhi mahitaji ya ndani aliye tumboni na kutoa
maziwa mengi baada ya kuzaa.
Mambo ya kuzingatia ni pamoja na
- Ng’ombe
apewe lishe bora na maji ya kutosha kipindi chote cha mimba
- Miezi
2 kabla ya kuzaa apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku
- Apewe
kinga dhidi ya maambukizi na tiba ya magonjwa
- Ng’ombe
anayekaribia kuzaa, hususani mtamba, azoeshwe kuingia kwenye sehemu ya
kukamulia.
DALILI
ZA NG’OMBE ANAYEKARIBIA KUZAA
Mfugaji anapaswa kufahamu dalili za
ng’ombe anayekaribia kuzaa ili aweze kufanya maandalizi
muhimu. Dalili hizo ni pamoja na
Kujitenda kutoka
kwa wenzake
Kiwele
kuongezeka
Chuchu kutoa
maziwa zikikamuliwa
Kutokwa na ute
mwekundu na sehemu za uke kuvimba na kulegea
Kuhangaika kulala
chini na kusimama na
Kati ya saa moja hadi mbili kabla ya kuzaa
sehemu ya uke hutokwa na maji mengi ambayo husaidia kulainisha njia ya ndama
kupita.
HUDUMA KWA NG’OMBE ANAYEZAA
Ng’ombe anayezaa anahitaji uangalizi
wa karibu ili kuhakikisha usalama wa ng’ombe na ndama
anaezaliwa. Mambo ya kuzingatia ni pamoja na yafuatayo:-
- Sehemu
ya kuzalia ng’ombe iandaliwe kwa kuwekwa nyasi kavu na laini na iwe safi.
- Ng’ombe
ahamishwe sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzaa mara baada ya dalili za kuzaa
kuonekana na
-Ng’ombe
aachwe azae mwenyewe bifa usumbufu
MFUGAJI APATE USHAURI/HUDUMA KUTOKA
KWA MTAALAM IWAPO MATATIZO YAFUATAYO YATAJITOKEZA:-
- Ng’ombe
kushindwa kuzaa kwa masaa mawili hadi matatu baada ya chupa kupasuka
-Kondo
la nyuma kushindwa kutoka masaa sita baada ya kuzaa
-Kizazi
kutoka nje na
-Ng’ombe
kushindwa kusimama baada ya kuzaa
MATUNZO YA NG’OMBE ANAYEKAMULIWA
Ng’ombe anayekamuliwa anahitaji
kupata chakula kwa ajili ya kujikimu na cha ziada kwa ajili ya uzalishaji wa
maziwa. Ili kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa maziwa ng’ombe
Apewe
chakula cha ziada kwa kiwango cha kilo 1 kwa kila lita 2 – 3 za maziwa
anayotoa.
Apewe
madini na virutubisho vingine kulingana na mahitaji
Apewe
maji mengi kwa vile ni ya muhimu katika kutengeneza maziwa.
Aachwe
kukamuliwa siku 60 kabla ya kuzaa. Uachishwaji huu ufanywe taratibu
ili ifikapo siku ya 60 kabla ya kuzaa ukamuaji usitishwe.
Baada
ya kusitisha kukamuliwa apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku hadi
atakapozaa
Apatiwe
kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa na tiba kulingana na ushauri wa mtaalam
wa mifugo.
UZALISHAJI WA MAZIWA
Lengo la ufugaji wa ng’ombe wa
maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na salama pamoja na mazao yatokanayo na
maziwa .
Mambo muhimu ya kuzingatia ni:-
-Sehemu
ya kukamulia iwe safi na yenye utulivu
-Ng’ombe
awe na afya nzuri msafi na kiwele kioshwe kwa maji safi ya uvuguvugu.
-Mkamuaji awe
msafi kucha fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza
-Inashauriwa
mkamuaji asibadilishwebadilishwe
-Vyombo
vya kukamulia viwe safi
-Muda
wa kukamua usibadilishwe
-Maziwa
ya mwanzo kutoka kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo maalum (strip cup) ili
kuchunguza ugonjwa wa kiwele.
UCHAGUZI WA UTUNZAJI WA DUME BORA LA
MBEGU
Dume ndilo linalojenga ubora wa
kundi la ng’ombe katika masuala ya uzalishaji kutokana na uwezo wake
wa kupanda majike 20 – 25 wakati wa msimu wa uzalianaji (breeding season).
Ili kundi la ng’ombe liwe bora,
mambo yafuatayo yazingatiwe
Chagua
dume kutoka kwenye ukoo ulio bora kwa kuzingatia kumbukubu za uzalishaji wa
maziwa au nyama za wazazi wake
Mfugaji
apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua dume bora
Lisha
dume malisho bora na maji safi ya kutosha. Pia apatiwe chakula cha
ziada.
Katika
ufugaji shadidi dume la ng’ombe lifugwe kwenye banda imara lenye
sehemu za kuwekea chakula maji na kufanyia mazoezi.
Dume
livalishwe pete puani kwa ajili ya kupunguza ukali na kuwezesha urahisi wa
kumshika.
Dume
apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingan ana ushauri wa mtaalam wa mifugo na
Mfugaji
apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua dume bora.
UTUNZAJI
WA NDAMA
-Wajengewe banda/boma imara safi na
lisilo na unyevunyevu ili kuepukana na magonjwa kama kichomi na kuhara
-Waruhusiwe kunyonya kwa muda
usiopungua miezi sita, pia wapatiwe majani laini kuanzia wanapofikia umri wa
wiki mbili ili waanze kula mapema.
-Wapatiwe maji safi na yakutosha
-Ndama dume ambao hawatahitajika kwa
ajili ya kuendeleza kizazi wahasiwe wakiwa na umri wa wiki mbili ili waanze
kula mapema.
-Wapatiwe maji safi na yakutosha
-Ndama dume ambao hawatahitajika kwa
ajili ya kuendeleza kizazi wahasiwe wakiwa na umri usiozidi miezi 3 ili wakue
haraka na kuwa na nyama nzuri.
-Wawekwe alama au namba za
utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya tano kwa ndama wote, mfano kuvalishwa
hereni kwenye masikio, kwa ajili ya urahisi wa udhibiti wa umiliki na utunzaji
kumbukumbu.
-Ndama wachungwe eneo tofauti na
ng’ombe wakubwa kuepuka maambukizi ya minyoo na magonjwa na
UTUNZAJI
WA NDAMA BAADA YA KUACHISHWA KUNYONYA HADI KUPEVUKA (MIEZI 6 – 24).
Ndama wa umri huu anatakiwa apatiwe
- Malisho
bora na maji safi ya kutosha wakati wote
-Vyakula
vya ziada ili kukidhi mahitaji ya mwili (mifano ya vyakula mchanganyiko
imeonyeshwa kwenye jedwali Na. 3 ) na
-Tiba
na kinga dhidi ya magonjwa hususan kinga ya kutupa mimba (S19) kwa ndama jike
watakaotumika kuendeleza kundi.
Katika kipindi cha miezi 6 hadi 24
mfugaji anashauriwa kuchagua ndama watakaoingizwa katika kundi la wazazi na
wanaobaki wawe katika kunenepesha kwa ajili ya nyama.
UZALISHAJI NA UHIFADHI WA MALISHO
BORA NA VYAKULA VYA ZIADA
Chakula kikuu cha ng’ombe ni nyasi,
vyakula vingine ni pamoja na miti malisho, mikunde na mabaki ya
mazao. Ili kupata malisho misimu yote ya mwaka ni muhimu kuvuna na
kuhifadhi malisho kipindi yanapopatikana kwa wingi. Inawezekana
kupanda malisho mengi kuliko kiasi kinachohitajika msimu mmoja/wakati wa mvua,
kuyavuna yanapofikia hatua ya kutoa maua na kuyahifadhi (mfano wa malisho
yanayoweza kupandwa ni mabingobingo, Guatemala, African fox-tail, desmodium,
centrosema, lukina n.k). Malisho yakupandwa ni vizuri yawe na
mchanganyiko wa jamii ya nyasi, mikunde na miti malisho.
MASALIA YA MAZAO SHAMBANI
Masalia ya mazao shambani kama vile
mabua, magunzi, majani ya mikunde, viazi, ndizi, mpunga, na mengineyo yanaweza
kukusanywa na kuhifadhiwa vizuri kama chakula cha ng’ombe.
MALISHO YA MITI NA MATUNDA YAKE
Malisho yatokanayo na miti ya
malisho na matunda yake yanaweza kutumika kama malisho ya
ng’ombe. Majani na matunda ya miti ya lukina, sesibania, migunga na
mbaazi yanaweza kukaushwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kulisha ng’ombe.
Mfano;mumea wa Lucina
VYAKULA VYA ZIADA
Ili kukidhi mahitaji ya viinilishwe
kulingana na kiwango cha uzalishaji, ng’ombe anatakiwa kupewa vyakula vya
ziada. Vyakula hivyo vinatokana na mchanganyiko wa vyakula
mbalimbali. Michanganyiko hii inategemeana na upatikanaji
wa malighafi katika maeneo husika. Mifano ya mchanganyiko huo ni
kama ifuatavyo:-
JEDWALI NA. 4 MFANO WA KWANZA WA
CHAKULA CHA ZIADA
AINA YA
CHAKULA
|
KIASI
(KILO)
|
Pumba za mahindi
|
47
|
Mahindi yaliyoparazwa
|
20
|
Mashudu ya alizeti/pamba
|
20
|
Unga wa lukina
|
10
|
Chokaa ya mifugo
|
2
|
Chumvi
|
1
|
Jumla
|
100
|
JEDWALI NA.5 MFANO WA PILI WA CHAKULA CHA ZIADA
Unga wa mahindi
|
Kilo 47
|
Pumba za mahindi
|
Kilo 3
|
Urea
|
Kilo 1
|
Mashudu ya alizeti
|
Kilo 2
|
Chumvi ya kawaida
|
Gramu 200
|
Unga wa mifupa
|
Gramu 200
|
Chokaa ya mifugo
|
Kilo 1.5
|
Saruji
|
Kilo 1
|
Mfugaji anatakiwa kuzingatia
yafuatayo ili kupata tija katika ufugaji:-
-kulisha
mchanganyiko wa nyasi, mikunde na mchanganyiko wa madini na vitamin
-kuvuna
nyasi na mikunde inapofikia hatua ya kutoa maua na kuyahifadhi kwa matumizi
wakati wa uhaba wa malisho hususan wakati wa kiangazi.
Mfano;Magugu maji
NJIA ZA KUHIFADHI MALISHO
Malisho yanaweza kuhifadhiwa kwa
kuyakausha (Hei) au kuyavundika (Sileji).Kwa matumizi ya kipindi cha kiangazi.
HEI
Hei ni majani yaliyohifadhiwa kwa
kukaushwa baada ya kukatwa au kuachwa kukauka yakiwa shambani kwa matumizi ya
baadaye. Katika kutengeneza hei yafuatayo yazingatiwe:-
- vuna
malisho yanapoanza kutoa maua
- Yaanikwe
kwa siku 3 hadi 6 kutegemea aina ya malisho na hali ya hewa na yageuze mara 1
au 2 kwa siku ili yakauke vizuri.
-Yafungwe
katika marobota baada ya kukauka inawezekana kutumia kasha la mbao lenye vipimo
vifuatavyo:- Urefu sentimeta 75, upana sentimeta 45 na kina
sentimeta 35 au mashine na zana za kufunga marobota ya hei na
- Hifadhi
marobota juu ya kichanja ili kuzuia maji yasiingie unyevu na kuharibiwa na
wadudu.
SILEJI
Sileji ni majani yaliyokatwakatwa na
kuvundikwa. Madhumuni ya kuyavundika ni kuyawezesha kubaki na ubora
wake hadi wakati yatakapotumika katika kutengeneza sileji yafuatayo
yazingatiwe:-
Tengeneza
sileji kwa kutumia majani yenye sukari nyingi kama mahindi au mabingobingo na
mikunde, mabaki ya viwandani kama molasis,
Andaa
shimo au mfuko wa plastiki kulingana na kiasi cha majani yaliyovunwa.
Vuna
majani ya kuvundika katika umri wa kuanza kutoa maua. Endapo majani
yaliyovunwa ni teketeke yaachwe kwa siku moja yanyauke kupunguza kiwango cha
maji.
Katakata
majani uliyovuna katika vipande vidogovidogo,
Tandaza
majani uliyokatakata ndani ya shimo au mfuko katika tabaka nyembamba na
kushindilia ili kuondoa hewa yote.
Funika
shimo ulilojaza majani kwa plastiki ikifuatiwa na udongo.
Sileji
itakuwa tayari kutumika kuanzia siku 21 na
Sileji
iliyofunguliwa kwa ajili ya matumizi ifunikwe haraka iwezekanavyo ili kuzuia
kuharibika.
Sileji inaweza kubaki na ubora
katika shimo kwa muda mrefu kama haitafunguliwa na kuachwa wazi kwa muda mrefu.
UDHIBITI WA MAGONJWA YA NG’OMBE
Afya bora ya ng’ombe inatokana na
kuzingatia mambo yafuatayo:-
Ndama apate maziwa
ya awali (dang’a) ya kutosha kwa siku 3 – 4 baada ya kuzaliwa ili kuongeza
kinga ya magonjwa mwilini.
Chovya kitovu cha
ndama ndani ya madini joto (Tincture of Iodine) mara baada ya kuzaliwa kuzuia
kuvimba kitovu kutokauka au kutohudumiwa ipasavyo mara baada ya ndama
kuzaliwa. Kitovu huvimba na kutoa usaha hukojoa kwa shida na wakati
mwingine huvimba viungo.
Ndama apewe dawa
ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 kama atakavyoshauri mtaalam wa
mifugo. Minyoo huwashambulia ndama zaidi hasa wale wanao kula
majani.
Zingatia usafi wa
vyombo na banda epuka kumpa ndama maziwa yaliyopoa na machafu ili kuzuia
kuharisha.
Zingatia ujenzi wa
mabanda kuruhusu mzunguko wa hewa ili kuzuia ndama kupata ugonjwa wa
vichomi. Vichomi huwapata ndama wa umri wa miezi 5 au zaidi
wanaofugwa ndani katika mabanda machafu yasiyo na mzunguko wa hewa ya kutosha.
Ogesha ng’ombe
kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo ili kuua kupe wote wanaoleta magonjwa
yatokanayo na kupe (ndigana kali na baridi, kukojoa damu na maji moyo) na
mbung’o (ndorobo),Pia
Ng’ombe wapatiwe
chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali chanjo muhimu ni za ugonjwa wa kutupa
mimba, kimeta, ugonjwa wa miguu na midomo na chambavu.
Mfugaji anashauriwa kutoa taarifa
kwa mtaalam wa mifugo anapoona ng’ombe wake ana baadhi ya dalili zifuatazo:-
Joto
kali la mwili na manyonya kusimama
Amepunguza
hamu ya kula
Amezubaa
na kutoa machozi
Anasimama
kwa shinda na kusinzia
Anapumua
kwa shida na pua kukauka
Anatokwa
na kamasi nyingi
Anajitenga
na kundi
Anakonda
Anapunguza
utoaji wa maziwa ghafla
KUMBUKUMBU
NA TAKWIMU MUHIMU
Kumbukumbu ni taarifa au maelezo
sahihi yaliyoandikwa kuhusu matukio muhimu ya kila ng’ombe na shughuli zote
zinazohusiana na ufugaji. Mfugaji anashauriwa kuweka kumbukumbu na
takwimu muhimu katika shughuli zake za ufugaji wa
ng’ombe. Kumbukumbu zinamsaidia mfugaji kujua mapato na matumizi na
kufanya maamuzi sahihi kuhusu mifugo husika na mifugo husika na mazao
yake. Aidha humwezesha kuweka mipango ya shughuli
zake. Mfugaji anapaswa kuweka kumbukumbu muhimu zifuatazo:-
Uzazi
(uhimilishaji na matumizi ya dume, tarehe ya kupandwa, kuzaa kuachisha
kunyonya)
Kinga
na tiba
Utoaji
wa maziwa
Ukuaji
Idadi
ya ng’ombe kwa makundi – majike, ndama, mitamba, madume,maksai.
UFUGAJI BORA WA NGURUWE
Banda
Ukubwa wa banda unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa
mita 2.5 zitawaweka guruwe 8-10 wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike moja
na dume moja
Jinsi ya kutengeneza chakula cha nguruwe
Chakula cha nguruwe wadogo kilo 100.
Mahindi
|
30
|
Pumba ya mahindi
|
40
|
Mashudu
|
18
|
Dagaa
|
10
|
Chokaa
|
1.25
|
Premix
|
0.25
|
Chumvi
|
0.5
|
Total
|
100
|
UTARATIBU WA MATUNZO
SIKU YA 1-2
a) mara tu baada ya kuhakikisha kuwa mama nguruwe amekwisha maliza kuzaa,vitovu vyote vilivyo virefu zaidi ya cm 10 hukatwa.
b) kunyunyiza iodine kwenye vitovu vilivyokatwa.
c) kukata meno makali 8, juu manne na chini manne kwa kutumia mkasi maalumu wa kukata meno, katika ukataji huo tunakikisha kuwa ncha zimeondolewa kwa madhumuni kuzuia watoboetoboe chumu za mama yao.
d) huwa nyekundu, hii inasadia kuzuia kuuma mkia hapo watakatapoongezeka kidogo na hata baadaye, Baada ya kukata huweza kumyunyuzia iodine vidonda hivyo,
e) mama nguruwe wachanga anapewa chakula kidogo sana kama ½ kila iwapo kuna ulazima wa kufanya hivyo, la sivyo apewe maji tu basi.
SIKU YA 3
a) Nguruwe wachanga ni laziwa wapatiwe madini ya chuma (iron injection) na vitamin A, D, na E, madini ya chuma ni lazima katika mwili wa nguruwe wakati wa maisha yao, kama hauwezi kupata sindano au chuma cha kulamba (iron paste) kutoka dukani basi waweza kuchukua kidogo udongo ambao ni mwekundu.
Iron injection pia husaidia nguruwe kuwa na damu ya kutosha kwani nguruwe wadogo husumbuliwa sana na hukosefuwa damu kwa kuwachoma iron itasaidia huzalishaji wa damu,
SIKU YA 4
Mama aendelee kuongezwa chakula, hakikisha joto kwa watoto linatosha.
SIKU YA 5
Chakula cha mama kinaongezwa hadi kufikia kilo 2 ½ kwa siku, chakula hiki kinatakiwa kuongezwa kutokana na wingi watoto mama nguruwe aliyezaa, hivyo basi kila mtoto mmoja aliyezaliwa humfanya mama aongezwe ¼ kilo kwa siku
mfano nguruwe mwenye watoto 10; 3 + 10 x ¼ = kilo 5.5
Kwa kifupi ni kwamba
Juma la kwanza; Nguruwe apewe ½ ya chakula anachostahili kupata
Juma la pili; nguruwe apewe ¾ ya chakula chote anachostahili kupata kwa siku.
Juma la tatu; Nguruwe apewe chakula chote anachostahili kupata kwa siku, ukweli ni kwamba nguruwe anayenyonyesha anapaswa kupewa chakula kiasi atakacho kula mama na watoto zaidi ya 8.baada ya kuachishwa kunyonyesha mama nguruwe anatakiwa apewe kilo 3 – 4 kwa siku, kwa madhumuni kumwandaa.
NB;Vinguruwe inafaa kuhasi kuanzia sk 14 mpaka 21 au na kuendelea,waachishwe kunyonya kuanzia sk 56
Katika siku hii, mama nguruwe aondolewe kutoka katika chumba na kuacha watoto katika chumba waliokula nah ii ina faa zaidi, usije ukaondoa mama na kuacha mama, Katika siku hiyo nguruwe hapewi chakula chochote cha siku nzima isipokuwa maji kidogo sana kumtosha ili kumfanya hakaushe maziwa kama hatua ya kuzuia ugonjwa wa kuvimba chuchu/ kiwele.
Kama kuna huwezekano keso yake mama huyo apatiwe au anyweshwe dawaya minyoo na chakula cha huyo mama kinaongezwa hadi kilo 3 au 3.5 kwa siku kwaajili ya flushing up
Pia wapatie nguruwe wadogo dawa za minyoo.
SIKU YA 1-2
a) mara tu baada ya kuhakikisha kuwa mama nguruwe amekwisha maliza kuzaa,vitovu vyote vilivyo virefu zaidi ya cm 10 hukatwa.
b) kunyunyiza iodine kwenye vitovu vilivyokatwa.
c) kukata meno makali 8, juu manne na chini manne kwa kutumia mkasi maalumu wa kukata meno, katika ukataji huo tunakikisha kuwa ncha zimeondolewa kwa madhumuni kuzuia watoboetoboe chumu za mama yao.
d) huwa nyekundu, hii inasadia kuzuia kuuma mkia hapo watakatapoongezeka kidogo na hata baadaye, Baada ya kukata huweza kumyunyuzia iodine vidonda hivyo,
e) mama nguruwe wachanga anapewa chakula kidogo sana kama ½ kila iwapo kuna ulazima wa kufanya hivyo, la sivyo apewe maji tu basi.
SIKU YA 3
a) Nguruwe wachanga ni laziwa wapatiwe madini ya chuma (iron injection) na vitamin A, D, na E, madini ya chuma ni lazima katika mwili wa nguruwe wakati wa maisha yao, kama hauwezi kupata sindano au chuma cha kulamba (iron paste) kutoka dukani basi waweza kuchukua kidogo udongo ambao ni mwekundu.
Iron injection pia husaidia nguruwe kuwa na damu ya kutosha kwani nguruwe wadogo husumbuliwa sana na hukosefuwa damu kwa kuwachoma iron itasaidia huzalishaji wa damu,
SIKU YA 4
Mama aendelee kuongezwa chakula, hakikisha joto kwa watoto linatosha.
SIKU YA 5
Chakula cha mama kinaongezwa hadi kufikia kilo 2 ½ kwa siku, chakula hiki kinatakiwa kuongezwa kutokana na wingi watoto mama nguruwe aliyezaa, hivyo basi kila mtoto mmoja aliyezaliwa humfanya mama aongezwe ¼ kilo kwa siku
mfano nguruwe mwenye watoto 10; 3 + 10 x ¼ = kilo 5.5
Kwa kifupi ni kwamba
Juma la kwanza; Nguruwe apewe ½ ya chakula anachostahili kupata
Juma la pili; nguruwe apewe ¾ ya chakula chote anachostahili kupata kwa siku.
Juma la tatu; Nguruwe apewe chakula chote anachostahili kupata kwa siku, ukweli ni kwamba nguruwe anayenyonyesha anapaswa kupewa chakula kiasi atakacho kula mama na watoto zaidi ya 8.baada ya kuachishwa kunyonyesha mama nguruwe anatakiwa apewe kilo 3 – 4 kwa siku, kwa madhumuni kumwandaa.
NB;Vinguruwe inafaa kuhasi kuanzia sk 14 mpaka 21 au na kuendelea,waachishwe kunyonya kuanzia sk 56
Katika siku hii, mama nguruwe aondolewe kutoka katika chumba na kuacha watoto katika chumba waliokula nah ii ina faa zaidi, usije ukaondoa mama na kuacha mama, Katika siku hiyo nguruwe hapewi chakula chochote cha siku nzima isipokuwa maji kidogo sana kumtosha ili kumfanya hakaushe maziwa kama hatua ya kuzuia ugonjwa wa kuvimba chuchu/ kiwele.
Kama kuna huwezekano keso yake mama huyo apatiwe au anyweshwe dawaya minyoo na chakula cha huyo mama kinaongezwa hadi kilo 3 au 3.5 kwa siku kwaajili ya flushing up
Pia wapatie nguruwe wadogo dawa za minyoo.
Chakula cha kukuzia
Nguruwe mkubwa kilo 100.
Pumba za mahind
|
45
|
Mahindi yaliyosagwa
|
30
|
Mashudu ya alizeti/pamba
|
15
|
Dagaa
|
3
|
Damu iliyosagwa
|
5
|
Madini(pigmix)
|
2
|
Total
|
100
|
KuzalianaNguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku
114, ambazo hugawanyika kwa miezi 3, wiki 3 na siku 3. Nguruwe mmoja ana uwezo
wa kuzaa watoto 6 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza
kula chakula cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili.
Endapo nguruwe watapata matunzo mazuri, baada ya miezi 8 wanakuwa na uzito kati
ya kilo 50-70 na wanaweza kuuzwa.
MatunzoBaada ya nguruwe kuzaa anatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha na cha kutia nguvu ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku moja au mbili toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili
.............................................................................................................................................
MatunzoBaada ya nguruwe kuzaa anatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha na cha kutia nguvu ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku moja au mbili toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili
.............................................................................................................................................
Tags:
MBINU ZA UFUGAJI
