UFUGAJI NGURUWE KWA TIJA

Ufugaji nguruwe kwa tija                         
Banda Ukubwa wa banda unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa mita 2.5 zitawaweka guruwe 8-10 wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike moja na dume moja                                                                                                                                                                                 
Jinsi ya kutengeneza chakula cha nguruwe
Chakula cha nguruwe wadogo kilo 100.
Mahindi
30
Pumba ya mahindi
40
Mashudu
18
Dagaa
10
Chokaa
1.25
Premix
0.25
Chumvi
0.5
Total
100
UTARATIBU WA MATUNZO
SIKU YA 1-2
a) mara tu baada ya kuhakikisha kuwa mama nguruwe amekwisha maliza kuzaa,vitovu vyote vilivyo virefu zaidi ya cm 10 hukatwa.
b) kunyunyiza iodine kwenye vitovu vilivyokatwa.
c) kukata meno makali 8, juu manne na chini manne kwa kutumia mkasi maalumu wa kukata meno, katika ukataji huo tunakikisha kuwa ncha zimeondolewa kwa madhumuni kuzuia watoboetoboe chumu za mama yao.
d) huwa nyekundu, hii inasadia kuzuia kuuma mkia hapo watakatapoongezeka kidogo na hata baadaye, Baada ya kukata huweza kumyunyuzia iodine vidonda hivyo,
e) mama nguruwe wachanga anapewa chakula kidogo sana kama ½ kila iwapo kuna ulazima wa kufanya hivyo, la sivyo apewe maji tu basi.
SIKU YA 3
a) Nguruwe wachanga ni laziwa wapatiwe madini ya chuma (iron injection) na vitamin A, D, na E, madini ya chuma ni lazima katika mwili wa nguruwe wakati wa maisha yao, kama hauwezi kupata sindano au chuma cha kulamba (iron paste) kutoka dukani basi waweza kuchukua kidogo udongo ambao ni mwekundu.
Iron injection pia husaidia nguruwe kuwa na damu ya kutosha kwani nguruwe wadogo husumbuliwa sana na hukosefuwa damu kwa kuwachoma iron itasaidia huzalishaji wa damu,
SIKU YA 4
Mama aendelee kuongezwa chakula, hakikisha joto kwa watoto linatosha.
SIKU YA 5
Chakula cha mama kinaongezwa hadi kufikia kilo 2 ½ kwa siku, chakula hiki kinatakiwa kuongezwa kutokana na wingi watoto mama nguruwe aliyezaa, hivyo basi kila mtoto mmoja aliyezaliwa humfanya mama aongezwe ¼ kilo kwa siku
mfano nguruwe mwenye watoto 10; 3 + 10 x ¼ = kilo 5.5
Kwa kifupi ni kwamba
Juma la kwanza; Nguruwe apewe ½ ya chakula anachostahili kupata
Juma la pili; nguruwe apewe ¾ ya chakula chote anachostahili kupata kwa siku.
Juma la tatu; Nguruwe apewe chakula chote anachostahili kupata kwa siku, ukweli ni kwamba nguruwe anayenyonyesha anapaswa kupewa chakula kiasi atakacho kula mama na watoto zaidi ya 8.baada ya kuachishwa kunyonyesha mama nguruwe anatakiwa apewe kilo 3 – 4 kwa siku, kwa madhumuni kumwandaa.

NB;Vinguruwe inafaa kuhasi kuanzia sk 14 mpaka 21 au na kuendelea,waachishwe kunyonya kuanzia sk 56
Katika siku hii, mama nguruwe aondolewe kutoka katika chumba na kuacha watoto katika chumba waliokula nah ii ina faa zaidi, usije ukaondoa mama na kuacha mama, Katika siku hiyo nguruwe hapewi chakula chochote cha siku nzima isipokuwa maji kidogo sana kumtosha ili kumfanya hakaushe maziwa kama hatua ya kuzuia ugonjwa wa kuvimba chuchu/ kiwele.
Kama kuna huwezekano keso yake mama huyo apatiwe au anyweshwe dawaya minyoo na chakula cha huyo mama kinaongezwa hadi kilo 3 au 3.5 kwa siku kwaajili ya flushing up
Pia wapatie nguruwe wadogo dawa za minyoo.
 Chakula cha kukuzia Nguruwe mkubwa kilo 100.
Pumba za mahind
45
Mahindi yaliyosagwa
30
Mashudu ya alizeti/pamba
15
Dagaa
3
Damu iliyosagwa
5
Madini(pigmix)
2
Total
100
 KuzalianaNguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114, ambazo hugawanyika kwa miezi 3, wiki 3 na siku 3. Nguruwe mmoja ana uwezo wa kuzaa watoto 6 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza kula chakula cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili. Endapo nguruwe watapata matunzo mazuri, baada ya miezi 8 wanakuwa na uzito kati ya kilo 50-70 na wanaweza kuuzwa.
MatunzoBaada ya nguruwe kuzaa anatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha na cha kutia nguvu ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku moja au mbili toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwil
 MATUNZO  NA UKUZAJI WA NGURUWE WACHANGA
Siku 1 mpaka 4 nguruwe wananyonya kutoka kwa mama maziwa yaitwayo COLOSTRUM, Ndani ya maziwa ya mwanzo hayo nguruwe wachanga wajipatie Vitamini A pamoja na antibodi ambapo huwafanya nguruwe wadogo wasipatwe na maradhi kwa urahisi sana, zaidi ya hapa wanapata protini kwa wingi sana, Nguruwe hawa wananyonya kiasi chochote watakacho.


..................................................................................................................................................
Previous Post Next Post