*JE WAJUA MAGONJWA MUHIMU YA YANAYOSUMBUA KUKU*
*UGONJWA WA MDONDO/KIDERI (NEWCASTLE DISEASE)*
Ugonjwa huu huathiri kuku katika umri wowote na unapoingia kwenye kundi huweza kuua idadi kubwa ya kuku hao hadi kufikia 90%. Ndege wakubwa hustahimili kidogo kuliko wale wadogo kwasababu ya usugu mwilini (body immunity) uliojengeka kwa muda mrefu zaidi.
Kisababishi cha ugonjwa (Etiology)
Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha kirusi kiitwacho Avian paramyxovirus-1 na huenezwa kwa njia ya hewa na kugusana, kutokuwepo kwa usalama wa viumbe hai (biosecurity) katika shamba lako, uchafu unaoletwa na magari, viatu, vifaa vya kazi, ndege wa porini na watalii
*Dalili za kideri:*
Vifo vya ghafla muda mwingine bila hata kuonesha dalili.
kuvimba shingo na kichwa
Kupooza (paralysis) kwa bawa na miguu
Ute hutoka mdomoni na puani
Kuku walioathirika hupata kizunguzungu.
Kuharisha uharo wa kijani
Kuzubaa, kusinzia na mabawa kushuka
Kuzunguka kama vile ana kifafa
Utagaji hushuka na mayai kuwa na umbo lisilokuwa la kawaida (deformed eggs)
Zaidi ya 90% ya kuku huweza kufa
Kuku hufa kwa kupinda shingo
Tiba:
Ugonjwa huu hauna dawa zaidi ya chanjo tu, lakini unaweza kutumia TRIMAZINE 30% pamoja na Vitamini kwa kuku walioathirika.
Kinga:
🔅Ugonjwa huu ukitokea jitahidi kuwatenga kuku wagonjwa na kuku wazima.
🔅Zuia muingiliano wa kutoka banda moja kwenda banda lingine pia weka maji yenye dawa (Farmguard) mlangoni kabla ya kuingia bandani na hakikisha unakanyaga hayo maji yenye dawa.
🔅kideri kinauzuiwa kwa njia ya chanjo, chanja kuku wako kila baada ya miezi mitatu na mara nne kwa mwaka. (Fuata mtiririko sahihi wa chanjo ya kideri)
🔅Epuka kuingiza kuku wageni kutoka shamba usilolifahamamu na usilojua kuhusu historia ya chanjo
..............................................
Tags:
MAGONJWA
