Mbinu Bora za ufugaji wa kuku

https://www.animalscience.care/






UKWELI WA KUUFUATA
UKWELI MCHUNGU 
 kabisa na hoja za msingi kabisa kwamba ufugaji wenye tija ni chakula sahihi, chenye ubora na kwa gharama nafuu 

LAKINI 

Hiyo haitoshi peke ake kuwa mfugaji utakae pata mafanikio kwenye idara hii ya ufugaji, yapo mambo kadhaa yakuyazingatia na kuyafanyia kazi ili kufikia mafanikio 

1: Viumbe hai salama, BIOSECIRITY  weka sheria utakazo zisimamia kuzuia magonjwa yasiingie bandani kwako kwa urahisi. 

2: Banda bora. Litakusaidia kuwaweka kuku wako mahala sahihi watakapo pata hifadhi na kuwa huru (zingatia Hewa madirisha makubwa ya mwanga na hewa safi, Paa lisilopitisha maji, Sakafu inayo nyonya unyevu). 

3: Muhudumu 
Awe na uelewa wa kazi anayoifanya, awapende kuku, awahudumie kwa wakati na awe mwenye kujituma kuwachunguza kuku( APENDWE NA ATHAMINIWE). 

4: Mwanga 

Muhimu sana kwa kuku wanao tarajiwa kutaga na wale wanaotaga, NOTE, hata kama kuku atakula chakula kizuri, hataugua ila kama hata pata masaa sahihi ya mwanga basi uzalishaji wake hautafikia asilimia zinazo tarajiwa ( REJEA  KITABU CHA FUGA KUKU KITAALAMU BY Greyson Kahise ujifinze kwa undani). ni somo refu. 

5: Ushauri wa kitaalamu. 

Hiki ni kipengele muhimu sana kwenye ufugaji, Jiulize kwanini Makampuni au wazalishaji wakubwa wanaajiri watu wenye taaluma kisimamia miradi yao?? ni kwasababu ufugaji huhitaji miongozo sahihi.... KAMWE Usipuuze ushauri wa kitaalamu utakunufaisha( MUWAPE HESHIMA YAO na taaluma zao) 

6: PENDA KUJIFUNZA. 

Kila kada inamiongozo yake hivyo ili kusimamia mradi wako kiuhakika hakikisha unakua na uelewa wa mradi wewe binafsi kama msimamizi hasa kwa kuhudhuria SEMINA , MAKONGAMANO na kupata miongozo sahihi ya ufugaji ( VITABU- Fuga kuku Kitaalamu kita kufaa sana ) 

7: USIKATE TAMAA MAPEMA 

kama ingekua kila anae pata hasara kwenye biashara anaacha basi kusingekua na biashara duniani, ila watu wanakubali kuchukua HATARI/TAKE RISK ili uimarike kiufahamu na itakufaa sana , utakua umejua changamoto na ukisimama tena utazipunguza hatimae utafanikiwa vema 

Previous Post Next Post