Kuku wa Mayai

KUKU WA MAYAI
https://www.animalscience.care/
 ni kuku ambao vinasaba vyao huwawezesha kutaga mayai mengi kwa muda watakao fugwa 

Zipo aina nyingi za kuku wa mayai hapa nitataja baadhi 

Hy-line, Isa brown, Bavon brown, Lohman brown, Rhode Island n.k 

Idadi ya kuku kwa mita moja mraba 7-8 ndio inayo shauriwa sana 

Wanahitaji vyombo vya kutosha vya maji 

Vyombo vya chakula na maji 

Belly drinker 1 kuku 60-80 

Chicken /feeder drinker kubwa Lita 20 kuku 50-60 
https://www.animalscience.care/

Chicken  drinker/feeder ndogo lita 10 kuku 20-25 
Hii huwezesha kuku kupata maji ya kutosha 

NB : Kuku anatakiwa kunywa maji zaidi ya Mara mbili ya chakula anachokula kwakua zaidi ya 75% ya yai ni maji, ukipunguza maji wanapunguza kutaga ZINGATIA. 

Kuku wapewe chakula kwa ratiba sahihi iliyo zoeleka usibadilishe ratiba utawastress na wataounguza kutaga 

Mfano huwa unalisha saa 12 AM na 4PM hakikisha unawalisha kila Siku muda huo 

Kuku walishwe kwa mfumo wa gramu ili kuzuia kujaza mafuta au kutumia chakula kingi kuzalisha yai 1., kwa kawaida kuku mmoja wa mayai anatakiwa kukupa mayai 6-7.( Hyline) 

Kuku wana pitia stage 3 

Brooding wakiwa vifaranga mpaka wiki 4, 

Growing wiki 5 -17 na Production baada ya kuanza kutaga mayai 

Hivi vipindi vinatofautiana kiuangalizi na kipindi cha kutaga hutegemea vipindi hivi( Brooding au malezi ya vifaranga na Growing) 

Brooding zingatia 
Chakula, Joto, hewa safi, Mwanga, nafasi ya kukaa inashauriwa 40 chicks kwa 1m2( vifaranga 40-60 kwa mita 1 mraba) 

Growing 
Zingatia chakula, Mwanga , nafasi na Hewa safi kwakua hapa ndo kuku anakua anaandaa mfumo mzima wa mayai 

Wape kuku 
Starter kwa wiki 6/8 

Grower 7/8-17 au watakapo anza kutaga 

Layers mash baada ya kuokota yai nakuendelea 

Kuku wakianza kutaga nivema ukawapa masaa 16 ya Mwanga kama somo la mwanga linavoelekeza. 

Hawa kuku wapewe chanjo zote 

Siku ya 7na 21 Newcastle (ya maji au matone) 
Siku ya 14na 28 gumboro( Ya maji) 
Siku ya 30ndui(Ya bawa) 
Kila baada ya miezi 3 rudia chanjo ya Newcastle 
Wape dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu. 

Uza mayai na uweke akiba kwaajili ya kuingiza kuku wengine , tunashauri uingize kuku kwa kutofautisha rika hii itakusaidia kukuza mradi pia kuwawezesha wateja wako kupata huduma muda wote. 
Previous Post Next Post