FOWL POX/AVIAN POX (NDUI)
Habari wadau,leo kwa mara nyingine tena tunakutana tena darasani ktk muendelezo wetu wa kupeana chakula cha ubongo kuhusu mambo mbali mbali yahusuyo ufugaji na leo ntauzungumzia ugonjwa wa ndui au Avian/Fowl pox, huu ni ugonjwa utokanao na virus ambao hushambulia kuku,bata mzinga,njiwa,kanga n.k lakin leo haswaa tutawalenga kuku kwani miongoni mwa kesi nyingi nilizokutana nazo kipindi hiki zinawahusu kuku ingawa njia ntakazozitoa za kupambana na gonjwa hili zaweza tumika kwa ndege wote na zikasaidia kwa usahihi.
Ingawa wadau kadhaa tayar wametoa mchango wao kuhusu ugonjwa huu lakin nami nimeona sio vibaya nikashea nanyi pia kile nilicho nacho.

CHANZO:~Ndui ama Avian/Fowl Pox ni ugonjwa unaosababshwa na kirusi aina ya `pox`, ugonjwa huu hauna tiba ya moja kwa moja bali ila una chanjo, tunaweza tibu magonjwa nyemelizi kisha baadaye kuku akishapona anapatiwa chanjo, na huenezwa na mbu ama wadudu wengine wanao uma na kuruka endapo wamebeba virus wakimng`ata kuku bas wanamuambukiza na kuku wenyewe wao kwa wao wakidonoana vidonda au wakigusana na maji maji yenye virus na vidonda bas ugonjwa huenea.
DALILI:~ hupoteza hamu ya kula,kupungua uzito,homa kali,kutokea vipele sehemu zisizo na manyoya,ndani ya siku 7~14 vipele hupasuka na kuacha vidonda,mara nyingi vidonda hupelekea kuziba macho na vifo huweza tokea kwa kuku wadogo.
TIBA/MSAADA:~Ugonjwa huu hauna tiba cha kufanya kuku anayeugua atengwe na wengine ili kuzuia kuenea kwa maambukiz apewe chakula na mchanganyiko wa Otc 50, Multi vitamins na glucose kwa siku 5~7, sugua vidonda na safisha uchafu wote kisha pakaa mafuta ya samli/ng`ombe,alizet,utomvu wa aloe vera,glycerine n.k ili kulainisha ngozi na kuzuia athari kuendelea., baada ya siku 7~10 atapata nafuu ndpo apewe chanjo.
KUDHIBITI/CHANJO:~ Chanjo ya ndui inachanjwa mara 1 tu, Mimi binafsi chanjo huwa nachoma siku ya 35 yaan week ya 5 ingawa unaweza pia ukachoma siku ya 17 au baada ya miez 2, jitahid sanaa kuangamiza mazalia ya mbu kwa kufyeka vichaka, kufukia madimbwi lakin jitahid sanaaa kupanda mimea ya michai chai kuzunguka banda lako kwan harufu yake mbu hawaipendi na huikimbia.
Kitu ambacho wengi hawakifaham ni kwamba kuku huugua ndui mara 1 tu akipona kamwe haijirudii mwili unakua tayar umetengeneza kinga ya asili kupambana nao,
Kitu ambacho wengi hawakifaham ni kwamba kuku huugua ndui mara 1 tu akipona kamwe haijirudii mwili unakua tayar umetengeneza kinga ya asili kupambana nao,
Tags:
MAGONJWA