FAIDA ZA MLONGE LONGE
Faida za dawa za asili kwa wafugaji huonekana pale mfugaji atakapo tumia vizuri dawa hizo.
Kutumia dawa za asili kusikufanye ukaacha kuwapa kuku wako chanjo.
_Mlonge una vitamini A na C
_Mlonge hutibu:
• Mafua.
• Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
• Homa ya matumbo.
• Mafua.
• Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
• Homa ya matumbo.
Mlonge ni moja ya mti wenye faida sana kwa mfugaji tukiachana na kutibu unaweza utumia kama kinga zidi ya magonjwa nyemelezi.
Mlonge ni mti wa muhimu kwa wafugaji kuku kwa kutibu na pia unaweza utumia kwa kuku ili kiini cha yai kiwe cha njano.
Kwahiyo mfugaji hakikisha huu Mti katika mazingira yako haukosekani:
JINSI YA KUUTUMIA
1. Mlonge unaweza kuuanika kivuli kisha unatwanga unga wake unauchanganya kwenye chakula cha kuku.
2. Mlonge unaweza ukautwanga majani yake mabichi ukawa kama
kisavu, kisha ukihakikisha umesha utwanga vizuri utachanganya kwenye
chakula watakacho kuwa wana kula siku hiyo kuku.
3. Mlonge unaweza ukawafungia kuku majani yake ili waya donone.
4. Mlonge unaweza ukatwanga majani yake ukayachanganya kwenye maji ukawapa kuku wanywe( njia Hii hutumika Mara nyingi kama tiba)
FAIDA ZA MLONGE
_ Mlonge una vitamin A na C , Kwahiyo kuku wanao pewa mlonge watakingwa dhidi ya ugonjwa wa upungufu wa vitamin A.
_Kuku wanao taga wakipewa mlonge Mara kwa mara yai litakuwa na kiini cha njano
_ Mlonge hutumika kama tiba
_Kuku ukiwapa mlonge Mara kwa Mara utawakinga na magonjwa nyemelezi upungufu wa vitamn A,Fowl Cholera, Mafua nk.
_Kuku wanao taga wakipewa mlonge Mara kwa mara yai litakuwa na kiini cha njano
_ Mlonge hutumika kama tiba
_Kuku ukiwapa mlonge Mara kwa Mara utawakinga na magonjwa nyemelezi upungufu wa vitamn A,Fowl Cholera, Mafua nk.
Zoea kuwapa mlonge kuku wako Mara kwa Mara ili kuimarisha Kinga ya mwili.
Bila kusahau chanjo✅
.....................................
Tags:
DAWA ZA MIFUGO
