UFUGAJI SAMAKI AINA YA SATO


UFUGAJI SAMAKI AINA YA SATO

UFUGAJI SAMAKI SATO

UFUGAJI BORA SAMAKI AINA YA SATO


1.0 UFUGAJI WA SAMAKI

Ni kitendo cha kuzalisha samaki katika mabwawa, matenki au Mifereji kwa lengo la chakula au kujipatia kipato

1.1 UMUHIMU WA UFUGAJI WA SAMAKI

Ufugaji wa samaki unazo faida mbalimbali ambazo ni:-

Ø Kujipatia chakula bora na cha kutosha kwa ajiri ya familia na jamii.

Ø Njia bora ya kujiajiri na kujiongezea kipato kutokana na mauzo ya samaki.

Ø Hutoa fursa ya matumizi ya ardhi isiyofaa kwa ajili ya kilimo.

Ø Ufugaji wa samaki hutoa nafasi ya kilimo mseto cha samaki na mazao/mifugo kwa wakati mmoja katika eneo moja, hivyo kutoa mavuno mengi.

1.2.0 MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA UFUGAJI WA SAMAKI;

1.2.1Mtaji

Ø Mkulima anashauriwa kuhakikisha kuwa ana mtaji kabla hajaamua kufanya ufugaji wa samaki, kiwango cha mtaji kitategemea ukubwa wa mradi husika.

1.2.2 Soko

Ø Ni vyema kujua upatikanaji wa soko pamoja na washindani wako kabla ya kuanzisha shughuli hii, japo kwa nchi yetu soko la samaki ni kubwa sana, hii inatokana na uhitaji mkubwa wa samaki katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

1.2.3 Elimu

Ø Mkulima anapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu samaki na jinsi ya kufuga ili aweze kuendesha mradi kwa urahisi, hivyo mkulima anaweza kutafuta mtaalam kutoka vyuo vya serikali au binafsi.

1.2.4 Upatikanaji wa mbegu(vifaranga) pamoja na chakula.

Ø Mkulima anashauriwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbegu bora na chakula cha kutosha kwa ajili ya kulisha samaki.

1.2.5 Eneo la kufugia samaki

Ø Ni vyema pia kutafuta eneo zuri kwa ajili ya kuchimba bwawa la kufugia samaki kwa kuzingatia upatikanaji wa maji kwa wakati wote wa msimu wa ufugaji, aina ya udongo, usalama na upatikanaji wa miundombinu husika (barabara, nishati ya umeme).

2.0 AINA YA SAMAKI;

2.1 Utafiti umefanyika katika nchi nyingi na kuonelea kuwa samaki aina ya perege/ngege/sato [tilapia] anafaa kufugwa katika mabwawa kulinganisha na aina nyingine.

2.2 Samaki wa aina hii wana sifa nzuri sana kwani; huishi kwenye maji yenye joto la kadri katika nchi nyingi, wanaweza kuzaana kwa wingi katika mabwawa, hula majani na chakula kingine chochote kinachopatikana kwa urahisi shambani au nyumbani, hukua kwa haraka, uvumilia sana changamoto za bwawa hii ikiwa ni mabadiliko ya joto, hewa ya oksijeni, na pH, pia nyama ya samaki hawa ni tamu na yenye ladha nzuri.

2.3 Kuna aina nyingi za sato(tilapia) kama vile Sato mwekundu, Sato wa Msumbiji, Sato mweupe na Sato wa Mwanza.

Sato hawa hula mimea na majani, huhitaji chakula kingi na huzaana sana, wana doa moja kubwa kwenye pezi la mgongoni. Sato hawa hula vijimea vya plankiton, hukua kwa haraka na wana mistari kwenye mikia. Aina nyingine za samaki zimechanganyikana na kuwa machotara hivyo siyo rahisi kuwatambua.

2.4 Sato wa Mwanza ni moja kati ya aina ya tilapia inayoshairiwa kufugwa na wataalamu wengi kwa kuzingatia sifa mbalimbali tofauti na aina nyingine.

3.0 ENEO LINALOFAA KWA UFUGAJI WA SAMAKI AINA YA SATO:

3.1.1 Upatikanaji wa maji

3.1.1 Maji ni moja ya hitaji muhimu katika ufugaji wa samaki. Eneo litafaa kwa ufugaji wa samaki ni lenye maji ya kutosha kuendesha shughuli zote za ufugaji kwa kipindi husika.

3.1.2 Chanzo cha maji kwenye bwawa kinaweza kuwa; mto, mfereji wa kumwagilia, au chemi chemi. Bwawa linahitaji maji mengi na sio rahisi kujazwa na ndoo. Ili kuhakikisha kuwa bwawa linakuwa na maji ya kutosha muda wote, chanzo cha maji cha faa kuwa cha kuaminika.

3.1.3 Kama mkulima ana maji ya kujaza kwenye bwawa kwa msimu, inawezekana pia kufuga samaki. Lakini mkulima ahakikishe anapanda vifaranga vya samaki mwanzo wa msimu wa maji. Hii itatoa fursa kwa samaki kukua hadi kufikia kiwango cha kuvunwa kabla ya maji kukauka.

3.1.4 Kama wakulima wanatumia chanzo kimoja cha maji ni muhimu kuanzisha utaratibu ambao utawezesha wakulima wote kutumia maji hayo bila matatizo
..........................................................................................................................................


Previous Post Next Post