Sasa


Magonjwa ya kuku na tiba

VENT PROLAPSE

Kutoka kwa nyama ya ndani ya  sehemu ya haja kuja nje na mara nyingi huwa na rangi nyekundu.
Tatizo hili huwa tokea watu wengi sana, na huwa likiwepo katika maswali mengi leo acha tuliongelee hili
#CHANZO CHA TATIZO HII
Tatizo hili mara nyingi hukumba kuku wa mayai, broiler au aina nyingine tofauti na hizi:
_Kuku kulishwa chakula chenye protein nyingi
_Kuku mwenye uzito mdogo kutaga mayai
_Ukubwa wa mayai
_Ukosefu wa madini joto (calcuim) ambayo husababisha kuku kushindwa kusukuma mayai
#KWA KUKU BROILER
Tatizo hili ni mara chache sana kutokea kwa kuku wa nyama/ broiler
-Kuku wa nyama hupatwa  na tatizo hili kutokana na kupewa chakula chenye mchanganyiko usio sahihi(ratio) hii hupelekea kuku kushindwa kumeng'enya chakula kwa usahihi na kusababisha kuku kutoa kinyesi kigumu na kusabaabisha kutoka kwa nyama sehemu ya haja pale anapo jisaidia.
#TIBA
-Endapo tatizo hili litatokea Unashauri kutumia mafuta (ointment) kumpa huyu kuku hata matone matatu ili kuweza kulainisha mmeng'enyo..
_Kutumia mchanganyo sahihi kwa kuku sio chakula cha kuku wa mayai kuwapa kuku wa nyama au hata kuku wanyama kumpa kuku wa mayai..
-Kutumia njia ya kawaida kurudisha hiyo nyama iliyo toka nje safisha hiyo nyama kwa maji safi kisha rudisha ndani pole pole kwa kutumia kidole.
-Tumia  antibiotic mfano #Otc 20% changanya na #Electrolytes,
Kama ukiikosa #Electrolytes   tumia #antibiotic + #vitamin
Ahsante kwa leo tuishie hapo.
#Endelea kulike page
#Ku share
#Comment
#Alika marafiki wako wapende ukurasa huu twende sambamba.
Previous Post Next Post