Sasa


Ugonjwa ni nini?

Ugonjwa ni nini?

Ugonjwa ni nini? Ugonjwa ni mabadiliko kutoka katika afya ya kawaida ya mnyama/kuku.
 Hali hii hutokea pale
vimelea au vijidudu vinapoingia mwili wa mnyama, kwa kula vyakula vyenye sumu, au inapotokea kuna uhaba wa
lishe au madini mwilini.
Tofauti za muonekano kati ya kuku mwenye afya na kuku mgonjwa
Kuku m
Macho na sura angavu
Hupenda kula na kunywa maji
Pua zilizo safi, upanga na undu mwekundu, manyoyalaini na yaliyopangika vizuri
 Hupumua kwa utulivu
Sehemu ya kutolea haja huwa kavu
Kinyesi kikavu, cheupe na kisicho na rangi
Hutaga mayai kawaida

Huonekana mchovu na dhaifu
Hula na kunywa kidogo au zaidi ya kawaida
Hutoa kamasi puani, ute na matongotongo; manyoya
yaliyovurugika
Hupumua kwa shida na kwa sauti
Sehemu ya kutolea haja inakuwa na unyevunyevu na
kinyesi kuganda
Huharisha, kinyesi huwa na damu au minyoo
Hutaga mayai machache au husimama kutaga kabisa
Huwa na tabia ya kujitenga na wenzake katika kundi

Previous Post Next Post