TABIA
Sungura wakiwa wanyama wanaowindwa kwa ajili ya chakula
huchunguza kwa makini kubwa makazi yao mapya na pindi na pindi wanapopata
vitisho / hatari hutulia kimya na kutazama kwa makini. Uoni wa sungura ni
uwanja mpana na kwa kiasi kikubwa huweza hata kuona juu ya vichwa vyao hata
akiwa ndani sungura atatafiti hali ya anga
UZAZI
Jike la sungura wa Kizungu huwa hawatoi mayai mpaka baada ya
kupandwa. Uterasi yao imegawanyika sehemu mbili hivyo kupandana kunaweza
kuhusisha matendo kadhaa ambayo yaweza kusababisha mimba kadhaa kutoka kwa
madume tofauti. Dume la sungura huwa hawawezi kutoa shahawa wakati wa joto la
kiangazi (majira ya joto). Sungura jike hubeba mimba kwa siku 30 mpaka 32 na
kuzaa watoto 12 – 13. Wakati mwingine huweza kufikisha watoto 18
Sungura ni wanyama wala nyasi wanaokula hasa nyasi na majani ya magugu. Kwa bahati mbaya chakula chao huwa na kiai kikubwa cha selulozi ambayo ni kazi sana kumeng’enya. Sungura hutatua tatizo hili kwa kutoa aina mbili za kinyesi; kimoja huwa kigumu na kingine huwa kilaini na chenye kunata. Hiki cha pili laini na chenye kunata huliwa tena. Hivyo sungura hula vinyesi vyao badala ya kuwa kama ng’ombe na wanyamma wengine ambao hula baada ya kucheua ili kumeng’enywa ili kupata virutubisho zaidi.
Sungura haraka sana kwa nusu saa ya kwanza ya malisho, maranyingi mchana karibu na jioni, ikifuatia nusu saa nyingine ambapo hula kwa kuchagua sana chakula. Ni wakati huu pia ndio sungura atatoa kinyesi kigumu kama uchafu, ambacho yeye hatakila. Kama mazingira hayahatarishi sungura atabaki nje kwa masaa mengi. Akiwa nje ya shimo lake sungura huwa akila kile jinyesi chake laini na hii huonwa mara chache zaidi, sababu hula tu baada ya kukitoa. Kwa kawaida sungura kinyesi chake kati ya saa mbili asubuhi na sa kumi na moja jioni akiwa ndani ya shimo lake.
Kinyesi kigumu na kikavu mara nyingi hutolewa nje ya shimo na kama inavyofahamika na kuliwa tena. Huku kile laini hutolewa ndani ya shimo saa chache baada ys kula wakati ambao pia kinyesi kikavu kishatolewa.
....................................................................................................
Tags:
SUNGURA
