1.MAJI
Maji ni muhimu sana kwa
kuku wawapo bandani. Wape maji ya kutosha kila wakati unapoona
yanapungua/kuisha ili waendelee kuyeyusha chakula wanachokula Nna kupunguza
joto mwilini. Kumbuka;Kuku 1 anaweza kunywa hadi robo lita ya maji kwa siku. Kwa hiyo utawawekea kulingana na
wingi wao. Pata chombo kizuri ili uwaning’inizie juu kidogo kutoka usawa wa
ardhi. Hii itasaidia kupunguza uchafuzi wa maji na magonjwa yanayoenezwa kwa
njia ya maji.
Hakikisha kuwa maji ni safi na salama.
Hakikisha kuwa maji ni safi na salama.
2. CHAKULA.
Ni vema kutafuta vifaa
vizuri kwaajili ya kuwawekea chakula. Tafuta vyombo ambavyo utaweza
kuning’iniza/tundika juu kidogo kutoka chini kulingana na umri wa kuku. Hii
itasadia sana kupunguza uwezekano wa kutosambaa kwa magonjwa hasa yale
yanayoenezwa kupitia viatu tunvyo vaa tunapoingia bandani. Pia itasaidi sana
kupunguza chakula kinacho mwagika chini wakati kuku wanapokula.
Kwa mfugaji yeyote wa kuku anapaswa kuelewa kuwa chakula cha kuku ni ghali. Hivyo ni vema kufuata taratibu vizuri katika ulishaji na kutengeneza/kununua vyombo ambavyo kuku hataweza kumwaga chakula. Kumbuka kwamba kama vyombo siyo vizuri basi vitamwaga chakula kingi na hivyo kukuletea hasara.
Ili kuweza kupata mazao mazuri yenye faida, ni vema ununue chakula cha kuku madukani au utengeneze wewe mwenyewe kama nitakavyoeleza hapa chini ili uwape kuku wako chakula chenye viini lishe vyote muhimu kwa kuzingatia umri wa kuku ulionao. Kwa vifaranga, unaweza kuwawekea chakula chini kwenye magazeti/mifuniko ya ndoo/sahani. Baada ya siku 10 unaweza kuwawekea kwenye chombo maalum.
Namna ya kuandaa chakula cha kuku. Vyakula vya kuku vinapaswa kuwa na aina/viini lishe muhimu kama vile Protini, Wanga, madini na Vitamini. Vyakula hivyo vimegawanyika kama ifuatavyo;
· Vyakula vya kujenga mwili ni; Jamii ya kunde,samaki, dagaa,mashudu ya
ufuta/alizeti/pamba,
· Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi
ni; Mafuta ya samaki na majani
mabichi kama vile; kabichi, mchicha,majani ya mpapai na nyasi mbichi.
· Vyakula vinavyojenga mwili/mifupa ni kama
vile; Aina za madini, chokaa,
chumvi na mifupa iliyosagwa.
· Vyakula
vilivyotajwa vinaweza kumkuza vizuri kuku hadi uuzwaji/kuliwa kwake. Surghum
Larrymeal huzuia kudonoana, huboresha kiini cha yai na kuongeza mayai.
Changanya kg 1 kwa kg 50 za pumba.
Ukosefu wa madini kama fosforasi na kalsiam husababisha matege, vidole kukunjamana, kufyatuka kwa misuli ya magoti, kuwa kilema na kupofuka macho kwa kuku
Tags:
UFUGAJI KUKU