Mfahamu kuku bora wa kufuga

Vifaa na Vyombo Muhimu
Mfugaji anashauriwa kutumia vifaa na vyombo maalum ili kurahisisha na
kuboresha utunzaji wa makundi mbalimbali ya kuku. Vifaa na vyombo
vinavyohitajika kwa ajili ya kuwekea chakula na maji, kutagia mayai na
kupumzika vinapatikana kwenye maduka ya pembejeo za mifugo. Aidha,
mfugaji anaweza kutengeneza mwenyewe kwa kutumia malighafi zilizopo
kwenye mazingira yake.
 Uchaguzi wa Kuku Bora wa Kufuga
 Kuku wa Asili
Aina za kuku wa asili wanaopatikana  nchini  Tanzania ni pamoja na Kuchi
(Kuza), pori (Kishingo), Njachama, Kinyavu, Mbuni na Tongwe nchini  Msumbiji.
Mfugaji anaweza kuongeza uzalishaji kwa kuchagua kuku mwenye sifa
zifuatazo:-
v Uwezo wa kutaga mayai mengi (kati ya 15-200 katika mzunguko
mmoja wa utagaji
v  Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi,
v  Uwezo wa kustahimili magonjwa
v  Umbo kubwa na kukua haraka.

Previous Post Next Post