Darasa la ufugaji wa kuku wa Kisasa

ufugaji kuku wa kienyeji

DARASA LA UFUGAJI
Ukiwa mfugaji unaejifunza  unatakiwa kuanza na ufugaji mdogomdogo ili kupata kujua changamoto za ufugaji kwanza,Kwa kufanya hivi itakusaidia kupata uzoefu katika nyanja zifuatazo:
1. UTUNZAJI (MANAGEMENT)
Kwa kuanza na kiasi kidogo itakusaidia kujua ni ukubwa gani unafaa kwa kuku wangapi, ukiwa na kuku wangapi utalisha chakula kiasi gani, pia utapata uzoefu wa chanjo muhimu zinazohitajika hali ambayo itakurahisishia pindi utapoanza ufugaji mkubwa.

2. SOKO
Hapa tunalenga upatikanaji wa wateja wa bidhaa zako za mifugo, itakusaidia kujua wateja waliopo wanavutiwa na bidhaa ya aina gani, kwa mfano mayai utajua wanapenda mayai ya kiini cheupe au cha njano? Kwa kufaham wanchokihitaji utajua ufanye nini ili ukidhi wanachokihitaji.

3. CHANGAMOTO
Ukianza na ufugaji mdogo pia itakusaidia kujua changamoto zilizopo kwenye ufugaji na utajifunza ni jinsi gani ya kuzitatua au kukabiliananazo kabla  ya kuanza ufugaji mkubwa.


Previous Post Next Post