Ufugaji kuku ni biashara kama biashara nyingine,
kuna wafugaji wengi wanaingia gharama zisizo za lazima katika kufuga kuku hali
ambayo inawapelekea kupunguza faida yao na maranyingine hata kutopata faida
kabisa, hali hii inawakwaza wafugaji na wengine hukata tamaa kabisa ya kufuga.
Lakini
hayo yanasababishwa na wao wenyewe wafugaji bila wenyewe kujijua
Ngoja tukumbushane namna gani mfugaji anaweza
kuzikwepa gharama zisizo za lazima katika ufugaji ili aweze kupata faida mara
dufu.
Fanya
haya kuongeza faida katika ufugaji kuku:-
Vifaranga bora ni wale waliototolewa katika
wakati uliopendekezwa kitaalaam hali ambayo inamjenga kifaranga kuwa na kinga
asilia ya mwili ya kutosha, kwahiyo mfugaji anaweza kufuga hadi kufikia kuuza
bila kutumia dawa za kutibu ugonjwa wowote zaidi ya chanjo na dawa za kuanzishia
tu, hivyo ataokoa pesa nyingi za kumuita daktari na kununua madawa na faida
itaongezeka siku hadi siku.
Hapa tunakusudia usafi wa banda, vyombo vya
chakula na maji, maji ya kunywa na muhudumu mwenyewe. Kwani magonjwa mengi ya
kuku yanasababishwa na uchafu, hivyo uleaji ukiwa mzuri magonjwa hayatakuwepo
halikadhalika na na gharama za matibabu hazitakuwepo pia.
3. CHAKULA BORA
Mfugaji anatakiwa ahakikishe anapata chakula
bora kwa ajili ya kuku wake, chakula bora ni ambacho kimekingwa na magonjwa
yote na kinakuza kuku kwa wakati, lakin pia chakula bora ni kile ambaho
hakisababishi mazingira hatarishi katika banda kama vile kulowesha banda.
Chakula ambacho kinalowesha banda kina hatari ya kusababisha magonjwa
mbalimbali kama vile coccidiosis na typhoid, hali ambayo mfugaji ataingia
gharama za kutibu mara kwa mara na kununua maranda.
Ili upate soko la uhakika ni lazima uwe na tabia
ya kutafuta taarifa (search information), kwa kutafuta taarifa itakuwezesha
kujua hali ya soko iliyopo ili nawe uweze kujipanga. Na kama ukiwa unategemea
tu mtu wa tenga aje mara nyingi utakuwa unalalamikia soko, hali ambayo itakupa
stress na kuuza kuku wako kwa bei ya hasara. Ila kama unajua hali halisi ya
soko basi hata akija mtu wa tenga nyumbani hatokudanganya na utakuwa na uhakika
na bei yako.
.....................................................................................................................
.....................................................................................................................
Tags:
UFUGAJI KUKU