NAMNA YA KUTUNZA KUMBUKUMBU KATIKA UFUGAJI WA KUKU :
Kwa mfugaji yeyeote yule wa kuku ni lazima aweze kujijengea utaratibu wa kuandika na kutunza kumbukumbu wa kuku wake. Usipo kuwa na utaraitibu huo, jiandae kusikia ule usemi usemao.”mali bila daftari hupotea bila habari“. Hivyo ni vyema ukiwa na mradi wowote wa ufugaji ni vema ukiwa unaweka kumbukumbu za kila siku au kwa kila wiki.KATIKA KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA UFUGAJI KUNA MAMBO MUHIMU YA KUYAZINGATIA KAMA IFUATAVYO:-
- Kumbukumbu za kuku na uzalishaji
kama ni kuku wa mayai basi kujua idadi ya mayai wanyotaga kila siku, ili uweze kujua asilimia za utagaji na uweze kupima kiwango chao cha utagaji.
- Kumbukumbu za chanjo.
- Kumbukumbu za afya.
- Gharama za vifaa na chakula.
MUHIMU: Njia rahisi ya kutunza kumbukumbu ni kununua daftari na kutengeneza majedwali yanayoonesha vipengele tajwa hapo juu