– TUNDA LINA VITAMINI ZIFUATAZO
1. Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri
2. Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve
3. Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa
4. Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili
5. Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi
6. Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu
MADINI – (MINERAL ELEMENTS)
Ni tunda lenye :
1. Madini ya Chuma kwa wingi (Fe) – Haya husaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxygeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi
2. Madini ya Calcium – Lina madini ya calcium, yanayosaidia kama ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili
3. Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa katika ufanyaji kazi mzuri wa selli hai za mwili
2. *AGRONOMY YA PARACHICHI (HALI YA HEWA)*
– Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, Kagera linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa
JOTO : Nyuzi 15-25 Sentigrade
MUINUKO : Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi
*UDONGO* : *Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji*
*AINA ZA PARACHICHI*
1. Zipo aina za kiasili : Kila sehemu kuna aina za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parachichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache
2. Zipo aina za kisasa (Chotara) : Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania
i. *HASS*
HASS AVOCADO
– Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi
– Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
– Limechongoka juu na chini
– Linahifadhika kwa urahisi
ii. Aina ya pili ni FUERTE
– Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
– Liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
– Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu
*FUERTE AVOCADO*
– Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo
iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania inaitwa X- ikulu
– Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
– Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
– Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
– Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana.
UPANDAJI WA PARACHICHI
NAFASI KATI YA SHIMO NA SHIMO NA IDADI YA MICHE KWA EKA.
– Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
– UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7 kwa vipimo hivyo utapanda miche 100 kwa heka 1 ambapo muda huo kila mti unakuwa umefikia mavuno yaliyokusudiwa patunda 600 hadi 800 kwa mti
MUDA WA KUPANDA
Wakati wa mvua ni muda mzuri wa kupanda ambao mvua za vuri zitanyesha mwezi wa 9 hadi 12.Mvua za masika ambazo zinanza mwezi 3. Ikiwa mkulima anaweza kumwagilia anaweza kupanda muda wowote wa mwaka
UKUBWA WA SHIMO LIWE BOX
– Au kipimo cha futi 2.5 x futi 2.5 x futi 2.5= sm 75 x sm 75 x sm 75
MBOLEA
– Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
– Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 40 au ndoo 2 za lita 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo *samadi ya ng`ombe nyeusi ambayo imeoza vizuri tokea kutolewa bandani ni mwezi na nusu*
KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO
– Parachichi hasa hizi za kisasa, hukomaa baada ya miezi 36
MAVUNO
– Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
– Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
– Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 7 hadi 8 unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa