SEHEMU YA KWANZA
Tikiti maji ni moja ya mmea wa matunda ambao umekuwa maarufu sana kipindi hiki, kibiashara na kwa matumizi ya chakula. Ni mmea huotao kwa kutambaa ardhini. Maua ya tikiti maji huchavushwa na wadudu hasa nyuki na huchukua takribani siku 65 mpaka 110 kutoka kusia mbegu mpaka kukomaa na hiyo hutegemea na aina, hali ya kimazingira/hewa na huduma.Inastawi vizuri katika aina mbalimbali za udongo wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji. Kiwango cha uchachu kinahitajika ni 5.0-6.8 ili kuiwezesha mimea kufyonza madini vizuri.Udongo wa kichanga mara nyingi huwa na uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na virutuisho vya mmea hivo umwagiliaji wa mara kwa mara na urutubishaji mzuri wapaswa kuzingatiwa ili kupata mavuno mazuri. Udongo wa mfinyanzi haupendekezwi sana lakini waweza leta mazao mazuri kama utamwagiliwa kwa umakini kuzuia maji yasituame hali inayoweza pelekea kutokeza kwa magonjwa.Tikiti maji huathiriwa sana na hali ya joto ya chini sana au lililozidi sana. Tikiti hupendelea hali ya hewa yenye joto (18-350 C) na mwangaza wa jua wa kutosha. Kiwango kidogo cha unyevu kwa sababu unyevu mwingi unasababisha maradhi na huweza kuathiri utamu wa matundaSEHEMU YA PILI Uoteshaji Tikiti maji huoteshwa kwa kupanda mbegu moja kwa moja shambani ambapo utapanda mbegu moja kwa kila shimo na unashauriwa kupannda kiasi kingine kidogo cha mbegu kwenye “seedling trays” ama kwenye viriba ili kuja kufidia mashimo ambayo mbegu zitashindwa kuota. Kwa tatizo kama hilo wengine hupanda mbegu mbili kwa kila shimo kwa hiyo basi mtu atumiaye njia hii atahitaji mbegu kiasi kikubwa zaidi ya aliyepanda mbegu moja kwa kila shimoNafasi na mahitaji ya mbeguhttps://www.kilimotrust.com/2020/10/kijue-kilimo-bora-cha-tikiti-maji-i.htmlUkubwa wa matunda unaohitajika ndio utakao eleza nafasi inayopaswa kuachwa katitati yamimea. Tikiti laweza pandwa kwa nafasi ya mita 0.6 mpaka mita 1 kutoka mmea mmoja kwenda mwingine na mita 0.9 mpaka mita 2 kutoka mstari moja kwenda mwingine Kwa wastani, ekari moja huhitaji kati ya gramu 400 mpaka gramu 700 kutegemea na nafasi ya kupanda itakayotumika.Urefu wa shimo la kupandia mbegu ni kuanzia sm 2 hadi sm 4. Kutegemea na hali ya joto ya eneo husika tikiti maji huchipua kuanzia siku 5 mpaka 10 Muda mpaka kukomaa/kuvunaKwa mbegu nyingi za hybrids tikiti maji huchukua siku 60 mpaka siku 85 kutoka kupandwa hadi kukomaa kutegemeana na hali ya joto na huduma………………………………………………………………………………………………………………………….
Tags:
AGRICULTURE