Zifuatazo ni faida zipatikanazo na ufugaji wa ng’ombe
- Chakula kama vile maziwa na nyama
- Mbolea
- Ngozi ambayo hutumika kama malighafi kutengeneza, viatu, mikanda, mikoba, nguo na vitanda
- Kujipatia pesa, pia ni akiba
- Ufahari na huongeza heshima kwa baadhi ya makabila.
- Kupata mapambo kama pembe
Uthibiti madhubuti wa magonjwa mbalimbali
Ili ng’ombe akue vizuri, akupe maziwa mengi na awe na afya nzuri zingatia yafuatayo;
- Uchaguzi wa ng’ombe mzuri wa kufuga
- Malisho mazuri tangia akiwa ndama
- Banda zuri
Chakula ni kitu muhimu kwa mifugo yote. Ulishaji wa ng’ombe wa maziwa na wengine huanzia toka anapozaliwa (ndama) na ndipo atakapo kuwa na mafanikio mazuri katika uzalishaji.
Ndama anapozaliwa tu anahitaji kupata maziwa ya kwanza (colostrum) kwa muda usiopungua siku tatu mfululizo.
Maziwa haya humsaidia kujikinga na magonjwa na pia humpatia ndama virutubisho vya kutosha. Baada ya hapo ndama aendelee kunywa maziwa ya mama mpaka atakapofikia mwezi mmoja, aanze kupatiwa chakula cha ziada (pumba ya mahindi iliyochanganywa na mashudu pamoja na majani mabichi yaliyokatwa katwa vipande vidogo vidogo).
Ndama akifikia umri kati ya miezi miwili na sita unaweza kumuachisha kunyonya, na anatakiwa apatiwe chakula chenye virutubisho sawa na maziwa ya mama.
Kwa mfano apatiwe pumba za mahindi zilizochanganywa na mashudu na majanimabichi (apatiwe wakati wote).
Ngombe jike wa kisasa hufikia umri wa kupandwa akiwa na mwaka mmoja na nusu. Ng’ ombe atakapokuwa na mimba ya miezi 7 kama alikuwa anakamuliwa anatakiwa kukaushwa na kupatiwa chakula chenye virutubisho zaidi.
Nyumba ya ng’ombe
Nyumba ni muhimu katika ufugaji wa ng’ombe. Tunashauriwa kuwahifadhi ng’ombe katika banda lenye hewa ya kutosha, lisilo na joto kali, lisilopitisha maji ya mvua na liwe lenye nafasi ya kutosha.
Pia banda la ng’ombe liwe na sakafu yenye mteremko kidogo kurahisisha usafi wa banda na kuzuia kutuama kwa maji na mkojo.
Nyumba ya ng’ombe inatakiwa iwe safi wakati wowote ili kuzuia magonjwa mbalimbali.
..................................................................

