VIZAZI VYA KUKU

https://www.animalscience.care/

NAPENDA KUTOA UFAFANUZI WA HILI SWALA 

Katika mnyororo wa vizazi vya kuku na wanyama wengine huwa kuna rank tangu kwa mababu mpaka kwa wajukuu. 

Leo naomba nielezee kuhusu 

Parental Stock, 
F1 
F2 

Parental Stock/wazazi 

Hawa ni kuku ambao vifaranga wao hupatikana kutaka kwa Grand parents/mabibi na mababu... 

Parental stock maranyingi huwa kwenye makampuni yanayo jihusisha na BREEDING au Breeders kwa jina jingine. 

Hawa maranyingi vifaranga wao huagiza nje, nchi tofauti kwa kutegemea aina ya kuku ambao wana wazalisha 


F1 First filial generation 

Hawa na vifaranga au kuku ambao wanazaliwa kutoka kwa kuku wazazi Parental stock huu ni uzao wa awali kabisa kutoka kwa kuku wazazi ambao huwa na Jogoo wa rangi Fulani na tetea wa rangi Fulani. 

 Mfano Vifaranga F1 wa kuku Hyline pure, jogoo mzazi huwa rangi ya Grey na Tetea huwa rangi nyeupe 

Ila kifaranga anaezalishwa Tetea huwa rangi Grey na jogoo huwa mweupe. 

Vifaranga F1 huwa na sifa bora za ukuaji kwa wale wanyama na za utagaji kwa wale wa mayai. 


F2 Second filial generation 

Huu ni kizaazi cha pili, na hutokana na mayai yanayo tagwa na kizazi cha kwanza yani F1 hawa pia huwa na ubora ila hushuka viwango vya ukuaji ukilinganisha na wale waliototolewa kutoka kwa wazazi( Parental Stock) 

Nimeona niliweke wazi hilo kwenu ili maswali kwangu kuhusu vifaranga yapungue... 

Wengi wamekua wakitangaza kuuza F1 siwezi kukanusha kwakua sijui wapi wanazalishia Ila kama mnunuzi unayo fursa ya kuulizawapi hawa wazazi au asili ya wazazi wa hao kuku wanatokea 

NB Ningumu kutambua vizazi vya kuku kwa kuangalia tu kwa macho, historia ya kuku kwa mzalishaji ndo inaweza kukupa ukweli kama ni F1 au F2 nk. 

Previous Post Next Post