TYPHOID /SALMONELOSIS

SALMONELA!!!! Typhoid 
https://www.animalscience.care/
Leo nizungumzie kuhusu huu ugonjwa sumbufu sana kwa wafugaji wengi na usiokua na huruma kwa wengi. 

Salmonella/typhoid/homa ya matumbo 

Huu ni ugonjwa unao wapata kuku wa rika zote kwa nyakati tofauti na umri tofauti, 

Ugonjwa huu huweza kuambukizwa kutoka kwa kuku mzazi kwenda kwenye yai na kupelekea kifaranga atakae zaliwa kuwa na ugonjwa huo (Pollourm) 

 NINI VYANZO HASA 
Mazingira yasiyo safi wanapoishi kuku 

Chakula chenye uchafu, uvundo au chenye vinyesi vya panya. 

Maji machafu au vyombo visivyo safi vya kuku. 

Kutoka kwa kuku wazazi 

Matumizi ya viambata visivyo kqushwa vizuri mfano Dagaa waliovunda, Damu iliyotoka kwa mfugo anaeumwa typhoid, magamba na mifupa isiyo salama( Chanzo cha uhakika cha malighafi ) 

Stoo yenye mpangilio mbaya , matundu yanayo ruhusu panya kuingia bandani. 

 DALILI 
Kuganda kwa kinyesi nyuma kilicho loana na cha rangi( Polurm kwa vifaranga) 

Kinyesi cheupe kama chokaa , au wakati mwingine kinyesi mchanganyiko bandani. 

Vifo visivyo koma, mfn leo1 kesho 2,,, vifo haviachi kutokea bandani ila hawafi kuku wengi sana kwa pamoja. 

Kuku hupoteza uzito kwa kiwango kikubwa (mfupa wa kifuani huwa umechongoka sana) 

Kuku wanaotaga kupunguza kutaga au kuacha kabisa kutaga( huathiri mfumo wa utengenezaji yai pia ) 

 SULUHISHO 

Chakula kisafi 

Mazingira safi ya banda 

Mpangilio wa stoo kuzuia Panya 

Nunua mayai au vifaranga kutoka kwenye shamba salama lisilo na ugonjwa. 

Vyakula unavyo wapa kuku kama DAMU, DAGAA,UDUVI, MIFUPA, KONOKONO viwe vimekauka na vihifadhiwe sehemu salama isiyo na unyevu. 

Watenge kuku wanaoonekana kuumwa au unaweza Fanya maamuzi magumu ya kuwauza kuku wote (SIO LAZIMA ITEGEMEE UKUBWA WA MTAJI WAKO) 

Baadhi ya dawa zinazo saidia kutibu Typhoid 
Trisul 
Trimafarm 
Esb3 
Ganadexel 
Enrovet 
Limoxin 

Ila kabla ya kujinunulia dawa wasiliana na Daktari alie karibu yako kubaini kama kweli unatibu TYPHOID/SALMONELLA. 

Kwa kifupi typhoid ikiingia bandani haiponi ikatoka moja kwa moja vimelea wanakuwepo bado jitahidi sana USAFI 
Maoni juu ya kupambana na PANYA 

Kwangua majani mita 2-3 kuzunguka banda au Fensi kuzuia panya kuingia bandani 

Zungusha mitego bandani amgalau kila baada ya mita 10 uwepo mtego wenye dawa 

Ziba mianya ya kuingia panya bandani 

Pangilia vizuri chakula stoo 


Previous Post Next Post