SOMO : KULEA VIFARANGA SEHEMU YA 2 MAANDALIZI YA KUPOKEA VIFARANGA.

Karibu ndugu mfugaji tuendelee pale  tulipo ishia hii ni sehemu ya 2maandalizi ya kupokea Vifaranga. 
Maandalizi kabla ya kupokea vifaranga : 
Inashauriwa vifaranga walelewe katika chumba maalum hadi umri wa majuma manne. 
Chumba kitayarishwe siku kumi na nne kabla ya vifaranga kuwasili kama ifuatavyo:
• Matundu yote yaliyo kwenye sakafu, dari, madirisha na ukuta yazibwe. 
• Kama chumba hicho kina sakafu ya saruji, kisafi shwe kwa maji ya moto na baadaye 
kinyunyizie dawa kama vile Rhino au Dettol ya kuua wadudu. Ikiwa chumba hicho 
hakina sakafu ya saruji, toa takataka zote kisha mwagia chokaa au majivu. 
• Mazingira ya nje ya banda yawekwe katika hali ya usafi ili kuzuia wadudu waharibifu. 
Kusafishwe hadi kufi kia upana wa mita mbili au zaidi kuzunguka banda. 
• Katika chumba watakamofi kia vifaranga tengeneza sehemu maalum ya kulelea 
(kitalu/bruda/brooder). 
Sehemu hiyo maalum inatakiwa iwe na umbile la duara, itengenezwe kwa 
kutumia box singbod nk. Kifaa hiki huhifadhi joto, huzuia upepo na huzuia 
vifaranga wasiende mbali na chanzo cha joto. 
• Sakafu iwekwe matandazo yaliyopigwa dawa mfano ya kuuwa wadudu kama Municipal 
disinfectant. Matandazo yaweza kuwa pumba ya mpunga, maranda ya mbao, maganda ya karanga n.k. 
Masaa mawili kabla ya kuwasili vifaranga vyenye umri wa siku moja taa au jiko liwashwe 
kwenye chumba cha kulelea vifaranga. 
Hii itasaidia chumba kuanza kupata joto la 
kutosha kuwawezesha vifaranga kula, kunywa bila shida. 
Vifaranga watakapo fika bandani wawepe kwanza glucose kwa muda wa masaa mawili. 
Baada ya masaa mawili kupita ndipo chakula kianze kuwekwa kwenye vyombo vya chakula 
na vifaranga waanze kula. 
MATUNZO BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA 
Hakikisha wanapata joto: 
Mfugaji anaweza kulea vifaranga wengi kwa kutumia Kitalu (bruda) unaoweza kutengenezwa 
kwa kutumia mbao au karatasi ngumu. 
_Vifaranga hujikusanya karibu nachanzo cha joto kama taa au 
jiko kujilundika katika sehemu moja kama joto ni kidogo. Hivyo ongeza joto kwa kushusha 
taa chini na kama bado joto litakuwa halitoshi, ongeza vifaa vya joto kama taa ya pili 
kutegemeana na hali halisi. 
Katika bruda/ kitalu cha kulea vifaranga mfugaji anatakiwa kufuatilia na kutambua kama 
hali ya joto iliyopo inawafaa vifaranga au la. 
 Ufuatiliaji wa karibu utamsaidia kuchukua hatua 
mapema endapo marekebisho yatahitajika. Hii utafahamu kwa kuangalia tabia ya vifaranga 
wanapokuwa ndani ya bruda 
 . 
Kama joto linatosheleza utaona yafuatayo 
 
• Vifaranga vitalia kwa furaha, 
• Vitakimbia kimbia, 
• Vitakunywa maji, 
• Vitachaguachagua takataka na 
• Kuonyesha shughuli nyingi, zote hizi ni dalili nzuri kuwa joto linatosha. 
Kama joto halitoshi utaona yafuatayo: 
•Vifaranga wakiona baridi , hujikusanya karibu 
zaidi na chanzo cha joto. 
• au wao wenyewe 
hujikusanya pamoja kwenye pembe ya bruda au 
nyumba na hulia kwa sauti. 
 Ukiona hivi ongeza 
kiwango cha joto adi waonekane kutawanyika 
kote kwenye bruda. 
Kama joto likizidi utaona yafuatayo 
 
• Vifaranga wakikaa mbali na vifaa vya joto ni 
 dalili kuwa joto limezidi. 
• Joto likiwa kali vifaranga hukimbia kutoka
 kwenye mwamvuli (kama umewekwa). 
• Husinzia na huzubaa. 
Katika hali hii itabidi upunguze joto kwa 
kupandisha taa juu na kama bado joto ni kali 
punguza vifaa vya joto na kuwapa vifaranga 
maji mengi ya kunywa. 
Kama kutakuwa na upepo unaopuliza 
kutoka upande mmoja utaona 
yafuatayo 
 
•Vifaranga watajikusanya upande mmoja wa 
kitalu/bruda mbali na upepo unakotokea. 
Kutegemeana na jinsi utakavyowaona vifaranga 
wanafanya, kama wataashiria tatizo, fanya 
marekebisho mapema kabla hayajatokea 
madhara kwa vifaranga. 
&Kumbuka:Katika majuma 5 ya kwanza vifaranga huhitaji joto usiku na mchana na 
katika majuma 3 yanayofuata joto hujitajiwa wakati wa usiku tu. 
Hata hivyo ikumbukwe kuwa joto katika nyumba ya vifaranga hubadilika kufuata maeneo 
tofauti na pia kutegemeana na majira tofauti ya mwaka. Hivyo kama hali ya baridi ikizidi, 
muda wa kuwasha taa urefushwe, wakati wa joto kali taa zinaweza kuzimishwa hata kama ni 
juma la kwanza au la pili. Jambo la msingi ni mfugaji kuwa macho na kuwapa vifaranga joto 
la kutosha mara tu hali ya hewa ikibadilika kuwa ya baridi ghafla. 
Hali ya hewa ikiwa nzuri madirisha yafunguliwe katika juma la kwanza au la pili kwa ajili ya 
kutunza matandazo sakafuni yasiwe na unyevu. 
Vifaranga huota manyoya mapya wakiwa na umri wa majuma 5 – 6 lakini huotesha manyoya 
ya kutosha katika juma la 8. Wakiisha ota manyoya ya kutosha vifaranga wanaweza kuvumilia 
zaidi hali ya baridi. Ufuatiliaji wa karibu ni muhimu kwa kipindi chote cha majuma matano (5) 
ili kuweza kuepusha vifo visivyokuwa vya lazima. 
Itaendelea........ 
Ulishaji Vifaranga 
Dawa 
Chanjo
Previous Post Next Post