MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE


MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE 

_Note_ 
Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. 

No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO 

_Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani 

_Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. 

Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. 

No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE 
_Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa 

Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus 

_Tiba_:Hakuna tiba ni ugonjwa wa virus. 

Chanja kuku wako Siku ya 14 na 28 

NO 3: MAREK'S DESEASE/ MAHEPE 
_Dalili kuu_:kuparalyse /kukakamaa kwa miguu na mbawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, 

 kuvimba kwa kiifadhia chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5/wakianza kutaga. 
_Tiba_:Hakuna tiba ni ugonjwa wa virus. 

Chanja vifaranga siku ya kwanza. 
https://www.animalscience.care/

NO 4: NDUI YA KUKU / FOWL POX. 
_Dalili kuu_:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya kama vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni. 

_Tiba_:Hakuna tiba ni ugonjwa wa virus, kupunguza madhara muoshe kwa maji ya uvugu vugu hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic kama Otc 20%. 

Chanja kuku wako Siku ya 30 au wiki ya .4 na 5( chanjo ni Mara moja ). Kwenye bawa 
https://www.animalscience.care/


No 5: MAFUA MAKALI/ CORYZA 
_Dalili kuu_:Chafya, kusinzia, kuvimba uso/kichwa /macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, urenda puani na mdomoni. 

_Tiba_: Fluban, au  tylodox au Enrovet dawa hizo pia ni vyema kuchanganya na vitamin. 
https://www.animalscience.care/

No 6: FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO 
_Dalili Kuu_:Mharo rangi ya nyeupe 
_Tiba_: Esb3, Trimazine 30%, Limoxin, enrovet, Ganadexel 
https://www.animalscience.care/


NO 7: COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU 
_Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu. 
_Tiba_: dawa nzuri ni Amprolium 20%,nyingine ni Esb3, Trimazine 30%, vitacox, na agracox 

Kuku wakifikia level ya kutoa damu tumia Anticox. 
https://www.animalscience.care/

NO 8: FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU 
_Dalili kuu_: kinyesi mharo wa kijani. 
_Tiba_: Tremazine 30 % au Esb3. 
https://www.animalscience.care/

MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKAN NA LISHE DUNI 
NO 9_Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana. 
_Tiba_: Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa vitamin, making, na protein, kwa wanaodonoana kata au choma midomo yao. 
Previous Post Next Post