UJUE UFUGAJI WA KUKU

 Swali: *Unadhani kwanini wafugaji wengi hurudi nyuma pindi waingiapo kwenye mradi wa kuku** 

 *Je?* 
👉Wanakua hawajajipanga vilivyo 
👉Wanakua na mategemeo makubwa kuliko uhalisia 
👉Changamoto zimewarudisha nyuma 
👉Wanafanya kwa mazoea na sikibiashara

Naomba chagua jibu unaloona kwako ni sahihi na ushauri nini kifanyike ili ufugaji wenye tija ufanyike 

Yafuatayo ni majumuisho ya maoni na ushauri kutoka kwa wadau wa sekta hii ya ufugaji kuku *(wafugaji, madaktari wa mifugo, nk)* 

Moja: *Soko la uhakika*, 
👉Asilimia kubwa ya wafugaji wametoa maoni kwamba kitu ambacho kimekua kikiwarudisha nyuma katika tasnia hii ya ufugaji kuku ni kukosa masoko baada ya kuzalisha, Malalamiko haya hasa yamewasilishwa na wafugaji wa kuku wa nyama na wanao zalisha mayai. 

 *Maoni juu ya ufumbuzi:* Serikali ione haja ya maksudi kuchukulia ufugaji kuku na kutambua bidhaa za kuku na kuzipa thamani kama bidhaa za wanyama wengine, Ziwepo bucha maalumu za kuchakata nyama kuongeza thamani, Pia pindi uzalishaji unapo zidi ione namna ya kuuhusu uuzwaji bidhaa nje ya nchi kuepusha hasara. 

Vyama vinavyo simamia sekta ya ufugaji vipewe meno, ya kutoa matamko juu ya bei za mauzo kwa kuzingatia gharama halisi za uzalishaji 

🔨 *Tunaamini humu wapo wafanyakazi wa sekta ya mifugo wizarani tusaidieni katika hili.* 

Mbili: *Changamoto zinazo jitokeza wakati mradi ukishaanza.* 
👉Wafugaji pia wameonesha kwamba changamoto kubwa zinazo warudisha nyuma ni *Magonjwa* na *Gharama za chakula* hivo pindi kuku wanapokufa kwa wingi, unapoteza mtaji na pengine kushindwa kuanza upya kwa kukata tamaa, au Gharama za uendeshaji mradi zinapokua zinapanda ghafla wengi huishia kupata hasara 

 *Utatuzi*: Ni vema wafugaji wawatumie wataalamu wanao waamini ili wanufaike 

Mazingira salama kwa kuku yawekwe kuwakinga na magonjwa ili kupunguza gharama za vifo na ununuzi wa madawa. 

Tuepuke kujipa mamlaka ya kuwa madaktari pasipo kujua magonjwa na utambuzi wake kitaalamu( *hii imepelekea wengi kutibu magonjwa yasiyo sahihi na hivo kuongeza vifo* ) 

Ili kupunguza gharama za uzalishaji, mfugaji azalishe mazao ambayo ni lazima kuyatumia kutengeneza chakula hasa , *Mahindi* na Kisha kupata *Formula* sahihi ya kutengeneza chakula. 

 Tatu: *Wafugaji wanakua hawajajipanga kikamilifu* 
👉Wafugaji wengi wamekua wakiingia kwenye ufugaji pasipo kuwa na ufahamu juu ya gharama halisi za mradi( *anafuga kwa nadharia)* Mfano, mfugaji alitarajia kutumia 500000, iwapo baada ya kuanza mradi atatakiwa kufikia 800000 nilazima ataona ufugaji ni gharama sana na atakata tamaa. 

 *Suluhu:* Kabla ya kuanza kufuga, mfugaji awasiliane na wafugaji wazoefu wampe maelekezo na changamoto halisi za mradi  wa kuku 

Mfugaji awe na andiko la mradi/business plan yenye uhalisia wa mradi impe picha halisi ya gharama za kuendesha mradi hasa kwa miezi mitano ya mwanzo kwa kuku wa mayai na chotara. 

NNE: *Matarajio makubwa kuliko uhalisia* 
👉Si vibaya kuwa na matarajio chanya juu ya mradi wowote unao ufanya, Ila matarajio kwenye mradi wa kuku yasijikite kutazama faida pekee kwa 100% , bali yawe nimatarajio ambayo yanauhalisia 

 *Mfn:* Mtu anaambiwa ukifuga kuku 300 huwezi kukosa tray 9-10, anaamini na anaweka pesa kwa matarajio hayo , wakati hapo uhalisia ni kwamba kuna kuku watakufa, wapo watakao chelewa kutaga,  na hivo matarajio hayatafikiwa, kama itatokea kutofikiwa wafugaji wanaokua na matarajio haya huona wanafuga kwa hasara na wengi hujitoa kwenye ugugaji, Hivo nibora kujua uhalisia wa mradi wa kuku. 

TANO: *Wafugaji kuku wengi wanafuga kimazoea* 
👉Takwimu zinaonesha asilimia kubwa ya wafugaji wadogo wamekua wakifuga pasipo kuzingatia miongozo maalumu ya ufugaji, na kwakua wengi hawafugi kibiashara hawaoni haja ya kuhudumia kuku ipasavyo 

👉 Wafugaji wengi huwahudumia kuku kwa uhakika hasa kwa mwezi mmoja au miwili ya kwanza baada ya hapo huwaacha kuku *yatima*  bila matunzo 

Hii hupelekea ukuaji hafifu wa kuku, au kukua kusiko na mpangilio na hatimae kuku huchelewa kukua na kuanza kutaga 

 *Suluhu* :Wafugaji tubadilike na kuanza kufuga, kibiashara kwa kuzingatia miongozo sahihi ya ufugaji 

Tuweke kumbukumbu za mradi , kwa mradi endelevu, tuwe wabunifu ili kukuza mradi wetu 

NB: *Tafuta elimu ya ufugaji kuku, bila kuchoka hata kwa gharama hii itakusaidia kupunguza sehemu kubw a ya changamoto* 

Uwe na mtaalamu wa kufuatilia mradi wako na umlipe kwa kazi hiyo, 

Kwa muhtasari katika mengi yaliyo jadiliwa nimeandika hayo kwa Leo 

 *Soma, elewa, zingatia, tumia ,elimisha wengine* 
Previous Post Next Post